Exodus 10:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Mose akamwambia, “Ni lazima uturuhusu kuchukua wanyama wa tambiko na sadaka za kuteketezwa ili tukamtambikie Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Musa akasema, “Huna budi kuturuhusu tuwe na dhabihu, na sadaka za kuteketezwa za kutoa mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa akasema, Ni lazima utupe mikononi mwetu na wanyama wa dhabihu na wa sadaka za kuteketezwa, ili tupate kumchinjia Bwana Mungu wetu dhabihu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Mose akamwambia, “Ni lazima uturuhusu kuchukua wanyama wa tambiko na sadaka za kuteketezwa ili tukamtambikie Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Mose akasema, “Huna budi kuturuhusu tuwe na dhabihu na sadaka za kuteketezwa za kutoa mbele za BWANA Mungu wetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Musa akasema, “Huna budi kuturuhusu tuwe na dhabihu na sadaka za kuteketezwa za kutoa mbele za bwana Mwenyezi Mungu wetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa akasema, Ni lazima utupe mikononi mwetu na wanyama wa dhabihu na wa sadaka za kuteketezwa, ili tupate kumchinjia BWANA Mungu wetu dhabihu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Mose akamwambia, “Ni lazima uturuhusu kuchukua wanyama wa tambiko na sadaka za kuteketezwa ili tukamtambikie Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mose akamwambia: Sharti wewe mwenyewe utupe mikononi mwetu ng'ombe za tambiko za kuchinja nazo za kuteketeza nzima, tupate za kumtolea Bwana Mungu wetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa akasema, Ni lazima utupe mikononi mwetu na wanyama wa dhabihu na wa sadaka za kuteketezwa, ili tupate kumchinjia BWANA Mungu wetu dhabihu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Musa akamwambia: “Unapaswa kuturuhusu kutwaa nyama wa matoleo na sadaka za kuteketezwa kwa kumutolea Yawe, Mungu wetu.