Exodus 10:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Mose na Aroni wakamwendea Farao na kumwambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Waebrania, anasema hivi, ‘Mpaka lini utakataa kujinyenyekesha mbele yangu? Waache watu wangu waondoke ili wapate kunitumikia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Musa na Haruni wakaenda kwa Farao na kumwambia, “Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Waebrania, asemalo: ‘Utaendelea hata lini kukataa kunyenyekea mbele yangu? Waachie watu wangu waende, ili waniabudu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, na kumwambia, Bwana, Mungu wa Waebrania, asema hivi, Je! Utakataa hata lini kujinyenyekeza mbele zangu? Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Mose na Aroni wakamwendea Farao na kumwambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Waebrania, anasema hivi, ‘Mpaka lini utakataa kujinyenyekesha mbele yangu? Waache watu wangu waondoke ili wapate kunitumikia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo Mose na Aroni wakaenda kwa Farao na kumwambia, “Hili ndilo BWANA, Mungu wa Waebrania, asemalo: ‘Utaendelea hata lini kukataa kunyenyekea mbele yangu? Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo Musa na Haruni wakaenda kwa Farao na kumwambia, “Hili ndilo bwana, Mungu wa Waebrania, asemalo: ‘Utaendelea hata lini kukataa kunyenyekea mbele yangu? Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, na kumwambia, BWANA, Mungu wa Waebrania, asema hivi, Je! Utakataa hata lini kujinyenyekeza mbele zangu? Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Mose na Aroni wakamwendea Farao na kumwambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Waebrania, anasema hivi, ‘Mpaka lini utakataa kujinyenyekesha mbele yangu? Waache watu wangu waondoke ili wapate kunitumikia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mose na Haroni walipofika kwake Farao wakamwambia: Hivi ndivyo, anavyosema Bwana Mungu wa Waebureo: Mpaka lini utakataa kujinyenyekeza usoni pangu? Watu hawa walio ukoo wangu wape ruhusa kwenda zao, wanitumikie!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, na kumwambia, BWANA, Mungu wa Waebrania, asema hivi, Je! Utakataa hata lini kujinyenyekeza mbele zangu? Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Musa na Haruni wakamwendea mufalme wa Misri na kumwambia: “Yawe, Mungu wa Waebrania, anasema hivi: ‘Mpaka wakati gani utakataa kujinyenyekeza mbele yangu? Uwaache watu wangu waondoke kusudi wanitumikie.