Exodus 10:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nzige hao watajaa katika nyumba zako, nyumba za maofisa wako na za Wamisri wote; watakuwa wengi kiasi ambacho hata wazee wenu hawajapata kuona tangu walipozaliwa, hadi leo.’” Basi, Mose akatoka kwa Farao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nzige hao watajaza nyumba zako, za maafisa wako wote na za Wamisri wote. Jambo ambalo baba zenu wala babu zenu hawajapata kuona tangu siku ile walipoanza kuishi katika nchi hii hadi leo.’ ” Ndipo Musa akageuka na kumwacha Farao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na nyumba zako, na nyumba za watumishi wako, na nyumba za Wamisri wote zitajawa na nzige; mfano wake baba zako wala baba za baba zako hawakuona, tangu siku walipoanza kuwapo juu ya nchi hata hivi leo. Basi akageuka na kutoka kwa Farao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nzige hao watajaa katika nyumba zako, nyumba za maofisa wako na za Wamisri wote; watakuwa wengi kiasi ambacho hata wazee wenu hawajapata kuona tangu walipozaliwa, hadi leo.’” Basi, Mose akatoka kwa Farao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nzige hao watajaza nyumba zako, za maafisa wako wote na za Wamisri wote. Jambo ambalo baba zenu wala babu zenu hawajapata kuona tangu siku ile walipoanza kuishi katika nchi hii mpaka leo hii.’ ” Ndipo Mose akageuka na kumwacha Farao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nzige hao watajaza nyumba zako, za maafisa wako wote na za Wamisri wote. Jambo ambalo baba zenu wala babu zenu hawajapata kuona tangu siku ile walipoanza kuishi katika nchi hii mpaka leo hii.’ ” Ndipo Musa akageuka na kumwacha Farao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na nyumba zako, na nyumba za watumishi wako, na nyumba za Wamisri wote zitajawa na nzige; mfano wake baba zako wala baba za baba zako hawakuuona, tangu siku walipoanza kuwapo juu ya nchi hadi hivi leo. Basi akageuka na kutoka kwa Farao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nzige hao watajaa katika nyumba zako, nyumba za maofisa wako na za Wamisri wote; watakuwa wengi kiasi ambacho hata wazee wenu hawajapata kuona tangu walipozaliwa, hadi leo.’” Basi, Mose akatoka kwa Farao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watajaa namo nyumbani mwako namo manyumbani mwa watumishi wako, namo manyumbani mwa Wamisri wote; ajabu kama hilo hawakuliona baba zako, wala baba za baba zako tangu hapo, walipoanza kuwapo katika nchi hii hata siku hii ya leo. Kisha akageuka, akatoka kwake Farao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na nyumba zako, na nyumba za watumishi wako, na nyumba za Wamisri wote zitajawa na nzige; mfano wake baba zako wala baba za baba zako hawakuona, tangu siku walipoanza kuwapo juu ya nchi hata hivi leo. Basi akageuka na kutoka kwa Farao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nzige wale watajaa katika nyumba zako, nyumba za wakubwa wako na za Wamisri wote. Watakuwa wengi kiasi ambacho hata wazee wenu hawajapata kuona tangu walipozaliwa, mpaka leo.’ ” Basi, Musa akatoka kwa mufalme wa Misri.