Exodus 10:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose akamjibu, “Kila mtu: Vijana na wazee, tutaondoka na watoto wetu wa kiume na wa kike, kondoo na mbuzi wetu na ng'ombe; kwa maana ni lazima tumfanyie sikukuu Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa akajibu, “Tutaenda na vijana wetu na wazee, pamoja na wana wetu na binti zetu, pia pamoja na mbuzi, kondoo, na ng’ombe wetu kwa sababu tutaadhimisha sikukuu kwa Mwenyezi Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa akamjibu, Tutakwenda na vijana wetu na wazee wetu, na wana wetu, na binti zetu, tutakwenda na kondoo zetu na ng'ombe zetu; kwa kuwa inatupasa kumfanyia Bwana sikukuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose akamjibu, “Kila mtu: vijana na wazee, tutaondoka na watoto wetu wa kiume na wa kike, kondoo na mbuzi wetu na ng'ombe; kwa maana ni lazima tumfanyie sikukuu Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose akajibu, “Tutakwenda na vijana wetu na wazee, pamoja na wana wetu na binti zetu, pia pamoja na kondoo zetu, ng'ombe, mbuzi, farasi na punda kwa sababu tutaadhimisha sikukuu kwa BWANA.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa akajibu, “Tutakwenda na vijana wetu na wazee, pamoja na wana wetu na binti zetu, pia pamoja na kondoo zetu, ng’ombe, mbuzi, farasi na punda kwa sababu tutaadhimisha sikukuu kwa bwana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa akamjibu, Tutakwenda na vijana wetu na wazee wetu, na wana wetu, na binti zetu, tutakwenda na kondoo zetu na ng'ombe zetu; kwa kuwa inatupasa kumfanyia BWANA sikukuu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose akamjibu, “Kila mtu: Vijana na wazee, tutaondoka na watoto wetu wa kiume na wa kike, kondoo na mbuzi wetu na ng'ombe; kwa maana ni lazima tumfanyie sikukuu Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mose akajibu: Tunakwenda vijana wetu na wazee wetu, wana wetu wa kiume na wa kike, nao mbuzi na kondoo wetu na ng'ombe wetu tutakwenda nao, kwani tuna sikukuu ya Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa akamjibu, Tutakwenda na vijana wetu na wazee wetu, na wana wetu, na binti zetu, tutakwenda na kondoo zetu na ng’ombe zetu; kwa kuwa inatupasa kumfanyia BWANA sikukuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa akamujibu: “Kila mutu, vijana na wazee, tutaondoka na watoto wetu wanaume na wanawake, kondoo na mbuzi wetu na ngombe. Kwa maana tunapaswa kumufanyia Yawe sikukuu.”