Exodus 11:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose akamalizia kwa kumwambia Farao, “Watumishi wako hawa watanijia na kuinama mbele yangu kwa heshima, wakinisihi niondoke nchini Misri, mimi pamoja na watu wote wanaonifuata. Baada ya hayo, nitaondoka.” Kisha Mose, huku akiwa ameghadhabika, akaondoka kwa Farao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maafisa hawa wako wote watanijia, wakisujudu mbele yangu, wakisema, ‘Ondoka, wewe pamoja na watu wako wote wanaokufuata!’ Baada ya haya nitaondoka.” Kisha Musa, akiwa amewaka hasira, akamwacha Farao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena hao watumishi wako wote watanitelemkia kwangu mimi, nao watanisujudia, wakisema, Toka wewe, na hawa watu wote wakufuatao; na baada ya hayo nitatoka. Basi akatoka kwa Farao na hasira kuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose akamalizia kwa kumwambia Farao, “Watumishi wako hawa watanijia na kuinama mbele yangu kwa heshima, wakinisihi niondoke nchini Misri, mimi pamoja na watu wote wanaonifuata. Baada ya hayo, nitaondoka.” Kisha Mose, huku akiwa ameghadhabika, akaondoka kwa Farao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maafisa hawa wako wote watanijia, wakisujudu mbele yangu, wakisema, ‘Ondoka, wewe pamoja na watu wako wote wanaokufuata!’ Baada ya haya nitaondoka.” Kisha Mose, huku akiwa amewaka hasira, akamwacha Farao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maafisa hawa wako wote watanijia, wakisujudu mbele yangu, wakisema, ‘Ondoka, wewe pamoja na watu wako wote wanaokufuata!’ Baada ya haya nitaondoka.” Kisha Musa, huku akiwa amewaka hasira, akamwacha Farao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena hao watumishi wako wote wataniteremkia kwangu mimi, nao watanisujudia, wakisema, Toka wewe, na hawa watu wote wakufuatao; na baada ya hayo nitatoka. Basi akatoka kwa Farao na hasira kuu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose akamalizia kwa kumwambia Farao, “Watumishi wako hawa watanijia na kuinama mbele yangu kwa heshima, wakinisihi niondoke nchini Misri, mimi pamoja na watu wote wanaonifuata. Baada ya hayo, nitaondoka.” Kisha Mose, huku akiwa ameghadhabika, akaondoka kwa Farao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, hawa watumishi wako wote watakapotelemka, waje kwangu na kuniangukia kwamba: Toka wewe na hawa watu wote wanaozifuata nyayo zako! Ndipo, nitakapotoka. Kisha Mose akatoka kwake Farao kwa kuwa na ukali uliowaka moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena hao watumishi wako wote watanitelemkia kwangu mimi, nao watanisujudia, wakisema, Toka wewe, na hawa watu wote wakufuatao; na baada ya hayo nitatoka. Basi akatoka kwa Farao na hasira kuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa akamalizia kwa kumwambia mufalme: “Watumishi wako hawa watanifikia na kuinama mbele yangu kwa heshima, wakinisihi niondoke katika inchi ya Misri, mimi pamoja na watu wote wanaonifuata. Nyuma ya hayo, nitaondoka.” Kisha Musa, akiwa amekasirika, akaondoka kwa mufalme wa Misri.