Exodus 12:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na hivi ndivyo mtakavyomla mnyama huyo: Mtakuwa mmejifunga mikanda viunoni mwenu, mmevaa viatu na fimbo zenu mikononi. Tena mtamla kwa haraka. Hiyo ni Pasaka ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivi ndivyo mtakavyokula: Mtajifunga mikanda viunoni, mtakuwa mmevaa viatu vyenu miguuni na kushika fimbo zenu mkononi mwenu. Mle kwa haraka; hii ni Pasaka ya Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na hivi ndivyo mtakavyomla mnyama huyo: mtakuwa mmejifunga mikanda viunoni mwenu, mmevaa viatu na fimbo zenu mikononi. Tena mtamla kwa haraka. Hiyo ni Pasaka ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivi ndivyo mtakavyokula: Mtajifunga mikanda viunoni, mtakuwa mmevaa viatu vyenu miguuni na kushika fimbo zenu mkononi mwenu. Mle kwa haraka; hii ni Pasaka ya BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivi ndivyo mtakavyokula: Mtajifunga mikanda viunoni, mtakuwa mmevaa viatu vyenu miguuni na kushika fimbo zenu mkononi mwenu. Mle kwa haraka; hii ni Pasaka ya bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni Pasaka ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na hivi ndivyo mtakavyomla mnyama huyo: Mtakuwa mmejifunga mikanda viunoni mwenu, mmevaa viatu na fimbo zenu mikononi. Tena mtamla kwa haraka. Hiyo ni Pasaka ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena hivi ndivyo, mtakavyozila: Viuno vyenu na viwe vimefungwa, namo miguuni mwe mmevaa viatu, nazo fimbo zenu na mzishike mikononi mwenu. Hivyo mzile kama watu wanaojihimiza kwenda safari. Kwani hii ndio Pasaka ya Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na hivi ndivyo mutakavyokula nyama yule: mutakuwa tayari kwa kusafiri, na kuvaa viatu na kuwa na fimbo zenu katika mikono. Tena mutamukula kwa haraka. Hiyo ni Pasaka ya Yawe.