Exodus 12:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vizazi hata vizazi mtaadhimisha tukio hilo kwa sikukuu kubwa kwa heshima yangu mimi Mwenyezi-Mungu. Hilo litakuwa agizo la milele kwenu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Siku hii itakuwa kumbukumbu kwenu, mtaiadhimisha kuwa sikukuu kwa Mwenyezi Mungu, katika vizazi vyenu vyote: mtalishika kuwa agizo la kudumu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa Bwana; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vizazi hata vizazi mtaadhimisha tukio hilo kwa sikukuu kubwa kwa heshima yangu mimi Mwenyezi-Mungu. Hilo litakuwa agizo la milele kwenu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Siku hii itakuwa kumbukumbu kwenu; mtaiadhimisha kuwa sikukuu kwa BWANA, katika vizazi vyenu vyote: mtaishika kuwa amri ya kudumu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Siku hii itakuwa kumbukumbu kwenu, mtaiadhimisha kuwa sikukuu kwa bwana, katika vizazi vyenu vyote: mtaishika kuwa amri ya kudumu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa BWANA; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vizazi hata vizazi mtaadhimisha tukio hilo kwa sikukuu kubwa kwa heshima yangu mimi Mwenyezi-Mungu. Hilo litakuwa agizo la milele kwenu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hiyo sharti iwe kwenu ya kuikumbuka, mwilie sikukuu ya Bwana. Haya na yawe maongozi ya kale na kale kwa vizazi vyenu vijvyo, mwilie sikukuu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa BWANA; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vizazi hata vizazi mutakumbuka tukio hilo kwa sikukuu kubwa kwa heshima yangu mimi Yawe. Hilo litakuwa agizo la milele kwenu.”