Exodus 12:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtaadhimisha sikukuu hii ya mikate isiyotiwa chachu kama ukumbusho wa siku nilipowatoa nyinyi, vikundi vya Israeli, kutoka Misri. Sikukuu hiyo itaadhimishwa na vizazi vyenu vyote vijavyo, kama agizo la milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mtaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, kwa sababu hiyo ndiyo siku ile niliyovitoa vikosi vyenu kutoka Misri. Mtaiadhimisha siku hii kwa vizazi vyenu vyote kuwa agizo la kudumu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi mtaitunza ile sikukuu ya mikate isiyochachwa; kwa kuwa katika siku iyo hiyo mimi nimeyatoa majeshi yenu katika nchi ya Misri; kwa hiyo mtaitunza siku hiyo katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtaadhimisha sikukuu hii ya mikate isiyotiwa chachu kama ukumbusho wa siku nilipowatoa nyinyi, vikundi vya Israeli, kutoka Misri. Sikukuu hiyo itaadhimishwa na vizazi vyenu vyote vijavyo, kama agizo la milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mtaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, kwa sababu hiyo ndiyo siku ile niliyovitoa vikosi vyenu kutoka Misri. Mtaiadhimisha siku hii kwa vizazi vyenu vyote kuwa amri ya kudumu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mtaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, kwa sababu hiyo ndiyo siku ile niliyovitoa vikosi vyenu kutoka Misri. Mtaiadhimisha siku hii kwa vizazi vyenu vyote kuwa amri ya kudumu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi mtaitunza ile sikukuu ya mikate isiyochachwa; kwa kuwa katika siku hiyo hiyo mimi nimeyatoa majeshi yenu katika nchi ya Misri; kwa hiyo mtaitunza siku hiyo katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtaadhimisha sikukuu hii ya mikate isiyotiwa chachu kama ukumbusho wa siku nilipowatoa nyinyi, vikundi vya Israeli, kutoka Misri. Sikukuu hiyo itaadhimishwa na vizazi vyenu vyote vijavyo, kama agizo la milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Iangalieni hiyo mikate isiyochachwa! Kwani siku hiyo ndipo papo hapo, nilipovitoa vikosi vyenu katika nchi ya Misri. Kwa hiyo iangalieni siku hiyo! Haya na yawe maongozi ya kale na kale kwa vizazi vyenu vijavyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi mtaitunza ile sikukuu ya mikate isiyochachwa; kwa kuwa katika siku iyo hiyo mimi nimeyatoa majeshi yenu katika nchi ya Misri; kwa hiyo mtaitunza siku hiyo katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutashika sikukuu hii ya Mikate Isiyotiwa Chachu kama ukumbusho wa siku nilipowatoa ninyi vikundi vya Israeli kutoka Misri. Sikukuu hiyo itashikwa na vizazi vyenu vyote vinavyokuja, kama agizo la milele.