Exodus 12:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika siku hizo saba, msiwe na chachu yoyote katika nyumba zenu. Mtu yeyote, awe mgeni au mwenyeji, akila kitu kilichotiwa chachu, ataondolewa miongoni mwa jumuiya ya Waisraeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa muda wa siku saba isionekane chachu yoyote katika nyumba zenu. Yeyote alaye chochote chenye chachu ndani yake, lazima akatiliwe mbali kutoka jumuiya ya Israeli, akiwa ni mgeni au mzawa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Muda wa siku saba isionekane chachu katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula hiyo iliyotiwa chachu, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na mkutano wa Israeli, akiwa mwenye kukaa hali ya ugeni, au akiwa mtu aliyezaliwa katika nchi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika siku hizo saba, msiwe na chachu yoyote katika nyumba zenu. Mtu yeyote, awe mgeni au mwenyeji, akila kitu kilichotiwa chachu, ataondolewa miongoni mwa jumuiya ya Waisraeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa muda wa siku saba isionekane chachu yo yote katika nyumba zenu. Ye yote alaye cho chote chenye chachu ndani yake, lazima akatiliwe mbali kutoka katika jumuiya ya Israeli, akiwa ni mgeni au mzawa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa muda wa siku saba isionekane chachu yoyote katika nyumba zenu. Yeyote alaye chochote chenye chachu ndani yake, lazima akatiliwe mbali kutoka jumuiya ya Israeli, akiwa ni mgeni au mzawa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Muda wa siku saba isionekane chachu katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu yeyote atakayekula hiyo iliyotiwa chachu, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na mkutano wa Israeli, akiwa mwenye kukaa kama mgeni, au akiwa mtu aliyezaliwa katika nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika siku hizo saba, msiwe na chachu yoyote katika nyumba zenu. Mtu yeyote, awe mgeni au mwenyeji, akila kitu kilichotiwa chachu, ataondolewa miongoni mwa jumuiya ya Waisraeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku saba chachu isionekane nyumbani mwenu, kwani kila atakayekula iliyo yenye chache siku hizo sharti huyo ang'olewe katika mkutano wa Waisiraeli, kama ni mgeni, au kama ni mzalia wa nchi hiyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Muda wa siku saba isionekane chachu katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula hiyo iliyotiwa chachu, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na mkutano wa Israeli, akiwa mwenye kukaa hali ya ugeni, au akiwa mtu aliyezaliwa katika nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku hizo saba, musikuwe na chachu yoyote katika nyumba zenu. Mutu yeyote, akuwe mugeni au mwenyeji, akikula kitu kilichotiwa chachu, ataondolewa katika kusanyiko la Waisraeli.