Exodus 12:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnamo usiku wa manane, Mwenyezi-Mungu aliwaua wazaliwa wa kwanza wote wa Misri. Wote walikufa, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao, mrithi wa ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa mfungwa gerezani. Hata wazaliwa wa kwanza wa wanyama nao walikufa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ilipofika usiku wa manane, Mwenyezi Mungu akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika Misri, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, mrithi wa kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa mfungwa, aliyekuwa gerezani, na wazaliwa wa kwanza wa mifugo yote pia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata ikawa, usiku wa manane Bwana akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa katika nyumba ya wafungwa; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnamo usiku wa manane, Mwenyezi-Mungu aliwaua wazaliwa wa kwanza wote wa Misri. Wote walikufa, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao, mrithi wa ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa mfungwa gerezani. Hata wazaliwa wa kwanza wa wanyama nao walikufa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ilipofika usiku wa manane, BWANA akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika Misri, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, mrithi wa kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa mfungwa, aliyekuwa gerezani, na wazaliwa wa kwanza wa mifugo yote pia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ilipofika usiku wa manane, bwana akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika Misri, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, mrithi wa kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa mfungwa, aliyekuwa gerezani, na wazaliwa wa kwanza wa mifugo yote pia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata ikawa, usiku wa manane BWANA akawaua wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hadi mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa katika nyumba ya wafungwa; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnamo usiku wa manane, Mwenyezi-Mungu aliwaua wazaliwa wa kwanza wote wa Misri. Wote walikufa, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao, mrithi wa ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa mfungwa gerezani. Hata wazaliwa wa kwanza wa wanyama nao walikufa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ulipokuwa usiku wa manane, Bwana akawapiga wana wa kwanza wote katika nchi ya Misri, kuanzia mwana wa kwanza wa Farao aliyekaa katika kiti chache cha kifalme, kuishia mwana wa kwanza wa mfungwa aliyekuwa chumbani kifungoni nao wana wote wa kwanza wa nyama wa kufuga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata ikawa, usiku wa manane BWANA akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa katika nyumba ya wafungwa; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katikati ya usiku, Yawe akawaua wazaliwa wa kwanza wote wa Misri. Wote walikufa, tangu muzaliwa wa kwanza wa mufalme wa Misri, murizi wa ufalme, mpaka muzaliwa wa kwanza wa mufungwa katika kifungo. Hata wazaliwa wa kwanza wa nyama nao walikufa.