Exodus 12:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Iambieni jumuiya yote ya Waisraeli kwamba mnamo siku ya kumi ya mwezi huu, mtachukua mwanakondoo mmoja kwa kila jamaa moja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Iambie jumuiya yote ya Israeli kwamba katika siku ya kumi ya mwezi huu, kila mtu atatwaa mwana-kondoo mmoja kwa ajili ya jamaa yake, mmoja kwa kila nyumba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Iambieni jumuiya yote ya Waisraeli kwamba mnamo siku ya kumi ya mwezi huu, mtachukua mwanakondoo mmoja kwa kila jamaa moja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Iambie jumuiya yote ya Israeli kwamba katika siku ya kumi ya mwezi huu, kila mtu atatwaa mwana-kondoo mmoja kwa ajili ya familia yake, mmoja kwa kila nyumba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Iambie jumuiya yote ya Israeli kwamba katika siku ya kumi ya mwezi huu, kila mtu atatwaa mwana-kondoo mmoja kwa ajili ya familia yake, mmoja kwa kila nyumba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Waambieni mkutano wote, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Iambieni jumuiya yote ya Waisraeli kwamba mnamo siku ya kumi ya mwezi huu, mtachukua mwanakondoo mmoja kwa kila jamaa moja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Uambieni mkutano wote wa wana wa Isiraeli kwamba: Siku ya kumi ya mwezi huu kila mwenye nyumba na achukue mwana kondoo, watu wa kila nyumba moja mwana kondoo mmoja!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muwaambie Waisraeli wote pamoja kwamba katika siku ya kumi ya mwezi huu, mutatwaa mwana-kondoo mumoja kwa kila jamaa moja.