Exodus 12:31 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Farao akawaita Mose na Aroni, usiku huohuo, akamwambia, “Amkeni! Ondokeni miongoni mwa watu wangu. Nendeni, nyinyi pamoja na hao Waisraeli, mkamtumikie Mwenyezi-Mungu kama mlivyosema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo Farao akawaita Musa na Haruni na kuwaambia, “Ondokeni! Tokeni kwa watu wangu, ninyi pamoja na Waisraeli! Nendeni mkamwabudu Mwenyezi Mungu kama mlivyoomba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaita Musa na Haruni usiku, akasema, Ondokeni tokeni katika watu wangu, ninyi na wana wa Israeli; enendeni, kamtumikieni Bwana kama mlivyosema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Farao akawaita Mose na Aroni, usiku huohuo, akamwambia, “Amkeni! Ondokeni miongoni mwa watu wangu. Nendeni, nyinyi pamoja na hao Waisraeli, mkamtumikie Mwenyezi-Mungu kama mlivyosema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo Farao akawaita Mose na Aroni na kuwaambia, “Ondokeni! Tokeni katika watu wangu, ninyi pamoja na Waisraeli! Nendeni mkamwabudu BWANA kama mlivyoomba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo Farao akawaita Musa na Haruni na kuwaambia, “Ondokeni! Tokeni kwa watu wangu, ninyi pamoja na Waisraeli! Nendeni mkamwabudu bwana kama mlivyoomba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaita Musa na Haruni usiku, akasema, Ondokeni tokeni katika watu wangu, ninyi na wana wa Israeli; nendeni, kamtumikieni BWANA kama mlivyosema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Farao akawaita Mose na Aroni, usiku huohuo, akamwambia, “Amkeni! Ondokeni miongoni mwa watu wangu. Nendeni, nyinyi pamoja na hao Waisraeli, mkamtumikie Mwenyezi-Mungu kama mlivyosema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akamwita Mose na Haroni usiku, akawaambia: Ondokeni, mtoke katikati yao walio ukoo wangu, ninyi na wana wa Isiraeli! Nendeni kumtumikia Bwana, kama mlivyosema!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaita Musa na Haruni usiku, akasema, Ondokeni tokeni katika watu wangu, ninyi na wana wa Israeli; enendeni, kamtumikieni BWANA kama mlivyosema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu mufalme wa Misri akaita Musa na Haruni, usiku uleule, akawaambia: “Musimame! Muondoke kati ya watu wangu. Muende, ninyi pamoja na wale Waisraeli, mumutumikie Yawe kama vile mulivyosema.