Exodus 12:34 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Waisraeli wakauchukua unga wao uliokandwa kabla haujatiwa chachu, na mabakuli yao ya kukandia wakiwa wamezifunga kwa nguo na kubeba mabegani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo watu wakachukua donge lao la unga kabla ya kutiwa chachu, wakaweka ndani ya mabakuli ya kukandia, wakayaviringisha katika mavazi na kuyabeba mabegani mwao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu wakauchukua unga wa mikate yao kabla haijatiwa chachu, na vyombo vyao vya kukandia wakavitia ndani ya nguo zao mabegani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Waisraeli wakauchukua unga wao uliokandwa kabla haujatiwa chachu, na mabakuli yao ya kukandia wakiwa wamezifunga kwa nguo na kubeba mabegani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo watu wakachukua donge lao la unga kabla ya kutiwa chachu, wakaweka ndani ya mabakuli ya kukandia, wakayaviringisha katika vitambaa na kuyabeba mabegani mwao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo watu wakachukua donge lao la unga kabla ya kutiwa chachu, wakaweka ndani ya mabakuli ya kukandia, wakayaviringisha katika vitambaa na kuyabeba mabegani mwao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu wakauchukua unga wa mikate yao kabla haijatiwa chachu, na vyombo vyao vya kukandia wakavitia ndani ya nguo zao mabegani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Waisraeli wakauchukua unga wao uliokandwa kabla haujatiwa chachu, na mabakuli yao ya kukandia wakiwa wamezifunga kwa nguo na kubeba mabegani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu wakauchukua unga wao uliokandwa, ukiwa haujachachuka bado, nayo mabakuli yao ya kukandia wakayafunga katika nguo zao, wakayachukua mabegani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu wakauchukua unga wa mikate yao kabla haijatiwa chachu, na vyombo vyao vya kukandia wakavitia ndani ya nguo zao mabegani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Waisraeli wakatwaa unga wao uliopondwa mbele haujatiwa chachu na mabakuli yao ya kupondea mikate walikuwa wamezifunga kwa nguo na kubeba juu ya mabega.