Exodus 12:42 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Usiku huo ambao Mwenyezi-Mungu alikesha ili kuwatoa Waisraeli nchini Misri, unapaswa kuadhimishwa na Waisraeli wote na vizazi vyao vyote, kama usiku wa kukesha kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliutenga usiku ule ili kuwatoa Waisraeli katika nchi ya Misri, basi Waisraeli wote wanapaswa kuadhimisha usiku huu kwa kukesha ili kumheshimu Mwenyezi Mungu katika vizazi vijavyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ni usiku wa kuangaliwa sana mbele za Bwana kwa sababu ya kuwatoa katika nchi ya Misri; huu ndio usiku wa Bwana, ambao wapasa kuangaliwa sana na wana wa Israeli wote katika vizazi vyao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Usiku huo ambao Mwenyezi-Mungu alikesha ili kuwatoa Waisraeli nchini Misri, unapaswa kuadhimishwa na Waisraeli wote na vizazi vyao vyote, kama usiku wa kukesha kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu BWANA aliutenga usiku ule ili kuwatoa Waisraeli katika nchi ya Misri, katika usiku huu Waisraeli wote wanapaswa kuadhimisha kwa kukesha ili kumheshimu BWANA katika vizazi vijavyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu bwana aliutenga usiku ule ili kuwatoa Waisraeli katika nchi ya Misri, katika usiku huu Waisraeli wote wanapaswa kuadhimisha kwa kukesha ili kumheshimu bwana katika vizazi vijavyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni usiku wa kuangaliwa sana mbele za BWANA kwa sababu ya kuwatoa katika nchi ya Misri; huu ndio usiku wa BWANA, ambao wapasa kuangaliwa sana na wana wa Israeli wote katika vizazi vyao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Usiku huo ambao Mwenyezi-Mungu alikesha ili kuwatoa Waisraeli nchini Misri, unapaswa kuadhimishwa na Waisraeli wote na vizazi vyao vyote, kama usiku wa kukesha kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Usiku huo wa kuwatoa katika nchi ya Misri ulikuwa usiku wa Bwana wa kuangaliwa; kwa hiyo usiku huo wa Bwana na uwe wa kuangaliwa kwa wana wote wa Isiraeli na kwa vizazi vyao vijavyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni usiku wa kuangaliwa sana mbele za BWANA kwa sababu ya kuwatoa katika nchi ya Misri; huu ndio usiku wa BWANA, ambao wapasa kuangaliwa sana na wana wa Israeli wote katika vizazi vyao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Usiku ule ambao Yawe alikesha kwa kuwatoa Waisraeli katika inchi ya Misri, unapaswa kukumbukwa na Waisraeli wote na vizazi vyao vyote, kama usiku wa kukesha kwa heshima ya Yawe.