Exodus 12:48 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mgeni yeyote anayeishi miongoni mwenu akipenda kuadhimisha sikukuu ya Pasaka, ni lazima kwanza wanaume wote wa nyumba yake watahiriwe; hapo atahesabiwa kuwa kama mwenyeji na kuruhusiwa kushiriki. Mwanamume yeyote asiyetahiriwa asishiriki kamwe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mgeni aishiye miongoni mwenu ambaye anataka kuadhimisha Pasaka ya Mwenyezi Mungu ni lazima wanaume wote waliomo nyumbani mwake wawe wametahiriwa, ndipo aweze kushiriki kama mzawa. Mwanaume yeyote asiyetahiriwa haruhusiwi kuila.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mgeni atakapoketi pamoja nawe, na kupenda kumfanyia Bwana pasaka, waume wake wote na watahiriwe, ndipo hapo akaribie na kufanya pasaka; naye atakuwa mfano mmoja na mtu aliyezaliwa katika nchi; lakini mtu ye yote asiyetahiriwa asimle.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mgeni yeyote anayeishi miongoni mwenu akipenda kuadhimisha sikukuu ya Pasaka, ni lazima kwanza wanaume wote wa nyumba yake watahiriwe; hapo atahesabiwa kuwa kama mwenyeji na kuruhusiwa kushiriki. Mwanamume yeyote asiyetahiriwa asishiriki kamwe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mgeni aishiye miongoni mwenu ambaye anataka kuadhimisha Pasaka ya BWANA ni lazima wanaume wote waliomo nyumbani mwake wawe wametahiriwa, ndipo aweze kushiriki kama mzawa. Mwanaume ye yote asiyetahiriwa haruhusiwi kuila.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mgeni aishiye miongoni mwenu ambaye anataka kuadhimisha Pasaka ya bwana ni lazima wanaume wote waliomo nyumbani mwake wawe wametahiriwa, ndipo aweze kushiriki kama mzawa. Mwanaume yeyote asiyetahiriwa haruhusiwi kuila.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mgeni atakapoketi pamoja nawe, na kupenda kumfanyia BWANA Pasaka, wanaume wake wote watahiriwe, ndipo hapo akaribie na kufanya Pasaka; naye atakuwa mfano mmoja na mtu aliyezaliwa katika nchi; lakini mtu yeyote asiyetahiriwa asimle.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mgeni yeyote anayeishi miongoni mwenu akipenda kuadhimisha sikukuu ya Pasaka, ni lazima kwanza wanaume wote wa nyumba yake watahiriwe; hapo atahesabiwa kuwa kama mwenyeji na kuruhusiwa kushiriki. Mwanamume yeyote asiyetahiriwa asishiriki kamwe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kama mgeni anakaa ugenini kwako, naye akitaka kuila Pasaka ya Bwana, uwatahiri wote walio wa kiume kwake, kisha ataweza kuikaribia kuila, maana atakua kama mzalia wa hiyo nchi, lakini kila asiyetahiriwa asiile!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mgeni atakapoketi pamoja nawe, na kupenda kumfanyia BWANA pasaka, waume wake wote na watahiriwe, ndipo hapo akaribie na kufanya pasaka; naye atakuwa mfano mmoja na mtu aliyezaliwa katika nchi; lakini mtu ye yote asiyetahiriwa asimle.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mugeni yeyote anayeishi kati yenu akipenda kushiriki sikukuu ya Pasaka, anapaswa kwanza kutahiri wanaume wote wa nyumba yake. Halafu atahesabiwa kuwa kama mwenyeji na kuruhusiwa kushiriki. Mwanaume yeyote asiyetahiriwa asishiriki hata kidogo.