Exodus 13:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
lazima kumwekea Mwenyezi-Mungu kila mzaliwa wenu wa kwanza wa kiume. Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mifugo yenu atakuwa wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
inakupasa kumtolea Mwenyezi Mungu kila mzaliwa wa kwanza. Wazaliwa wote wa kwanza wa kiume wa mifugo yako ni mali ya Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ndipo utamwekea Bwana kila afunguaye tumbo, na kila mzaliwa wa kwanza uliye naye, azaliwaye na mnyama; hao waume watakuwa ni wa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
lazima kumwekea Mwenyezi-Mungu kila mzaliwa wenu wa kwanza wa kiume. Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mifugo yenu atakuwa wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
inakupasa kumtolea BWANA mzaliwa wa kwanza wa kila tumbo. Wazaliwa wote wa kwanza wa kiume wa mifugo yako ni mali ya BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
inakupasa kumtolea bwana mzaliwa wa kwanza wa kila tumbo. Wazaliwa wote wa kwanza wa kiume wa mifugo yako ni mali ya bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ndipo utamwekea BWANA kila afunguaye tumbo, na kila mzaliwa wa kwanza uliye naye, azaliwaye na mnyama; hao wa kiume watakuwa ni wa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
lazima kumwekea Mwenyezi-Mungu kila mzaliwa wenu wa kwanza wa kiume. Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mifugo yenu atakuwa wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo umtolee Bwana kila atakayezaliwa wa kwanza na mama yake naye kila mwana wa nyama wa kufuga atakayekuwa wa kwanza, utakayempata, wao wa kiume watakuwa wake Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ndipo utamwekea BWANA kila afunguaye tumbo, na kila mzaliwa wa kwanza uliye naye, azaliwaye na mnyama; hao waume watakuwa ni wa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
munapaswa kumuwekea Yawe kila muzaliwa wenu wa kwanza mwanaume. Kila muzaliwa wa kwanza dume wa mifugo yenu atakuwa wa Yawe.