Exodus 13:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Farao kwa ukaidi alikataa kutuachia tuondoke; kwa hiyo Mwenyezi-Mungu alimuua kila mzaliwa wa kwanza nchini Misri, mzaliwa wa kwanza wa binadamu na wa mnyama. Basi, mimi ninamtolea sadaka Mwenyezi-Mungu kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mifugo yangu, lakini kila mzaliwa wa kwanza wa wanangu namkomboa.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Farao alipokataa kwa ukaidi kuturuhusu kuondoka, Mwenyezi Mungu aliua kila mzaliwa wa kwanza wa Wamisri, mwanadamu na wa mnyama. Hii ndiyo sababu ninatoa dhabihu kwa Mwenyezi Mungu mzaliwa wa kwanza wa kiume wa kila tumbo, na kumkomboa kila mzaliwa wa kwanza wa wana wangu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
basi ilikuwa hapo Farao alipojifanya kuwa mgumu ili asitupe ruhusa kuondoka, Bwana akawapiga wazaliwa wa kwanza wote waliokuwa katika nchi ya Misri, wa binadamu na wa mnyama; kwa ajili ya hayo namtolea Bwana wote wafunguao tumbo, wakiwa waume; lakini wazaliwa wa kwanza wote wa wana wangu nawakomboa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Farao kwa ukaidi alikataa kutuachia tuondoke; kwa hiyo Mwenyezi-Mungu alimuua kila mzaliwa wa kwanza nchini Misri, mzaliwa wa kwanza wa binadamu na wa mnyama. Basi, mimi ninamtolea sadaka Mwenyezi-Mungu kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mifugo yangu, lakini kila mzaliwa wa kwanza wa wanangu namkomboa.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Farao alipokataa kwa ukaidi kuturuhusu kuondoka, BWANA aliua kila mzaliwa wa kwanza wa Wamisri, mwanadamu na wa mnyama. Hii ndiyo sababu ninatoa dhabihu kwa BWANA mzaliwa wa kwanza wa kiume, wa kila tumbo na kumkomboa kila mzaliwa wa kwanza wa wana wangu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Farao alipokataa kwa ukaidi kuturuhusu kuondoka, bwana aliua kila mzaliwa wa kwanza wa Wamisri, mwanadamu na wa mnyama. Hii ndiyo sababu ninatoa dhabihu kwa bwana mzaliwa wa kwanza wa kiume, wa kila tumbo na kumkomboa kila mzaliwa wa kwanza wa wana wangu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
basi ilikuwa hapo Farao alipojifanya kuwa mgumu ili asitupe ruhusa kuondoka, BWANA akawapiga wazaliwa wa kwanza wote waliokuwa katika nchi ya Misri, wa binadamu na wa mnyama; kwa ajili ya hayo namtolea BWANA wote wafunguao tumbo, wakiwa wa kiume; lakini wazaliwa wa kwanza wote wa wana wangu nawakomboa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Farao kwa ukaidi alikataa kutuachia tuondoke; kwa hiyo Mwenyezi-Mungu alimuua kila mzaliwa wa kwanza nchini Misri, mzaliwa wa kwanza wa binadamu na wa mnyama. Basi, mimi ninamtolea sadaka Mwenyezi-Mungu kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mifugo yangu, lakini kila mzaliwa wa kwanza wa wanangu namkomboa.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Farao alipojishupaza, asitupe ruhusa kwenda zetu, Bwana aliwaua wana wote wa kwanza katika nchi ya Misri, wao waliokuwa wana wa kwanza wa watu nao waliokuwa wana wa kwanza wa nyama wa kufuga; kwa hiyo ninamtolea Bwana wana wao wote wanaozaliwa wa kwanza wa mama zao walio wa kiume, nao wana wa kwanza wa wanangu ninawakomboa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
basi ilikuwa hapo Farao alipojifanya kuwa mgumu ili asitupe ruhusa kuondoka, BWANA akawapiga wazaliwa wa kwanza wote waliokuwa katika nchi ya Misri, wa binadamu na wa mnyama; kwa ajili ya hayo namtolea BWANA wote wafunguao tumbo, wakiwa waume; lakini wazaliwa wa kwanza wote wa wana wangu nawakomboa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme wa Misri kwa ugumu wake alikataa kutuachilia tuondoke. Kwa hiyo Yawe akamwua kila muzaliwa wa kwanza katika inchi ya Misri, muzaliwa wa kwanza wa mwanadamu na wa nyama. Basi, mimi ninamutolea Yawe sadaka kila muzaliwa wa kwanza dume wa mifugo yangu. Lakini kila muzaliwa wa kwanza wa wana wangu ninamukomboa.’