Exodus 13:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati Farao alipowaachia Waisraeli waende zao, Mungu hakuwapitisha katika nchi ya Wafilisti, ingawa njia hiyo ilikuwa ya karibu. Mungu alisema, “Sipendi watu hawa wabadilishe nia na kurudi Misri wakijua itawabidi kupigana vita.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Farao alipowaachia watu waende, Mungu hakuwaongoza kufuata njia ipitayo katika nchi ya Wafilisti, ingawa njia hiyo ilikuwa fupi zaidi. Kwa maana Mungu alisema, “Wakikabiliana na vita, wanaweza kubadili mawazo yao na kurudi Misri.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ilikuwa hapo Farao alipokwisha kuwaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakaghairi watu hawa hapo watakapokutana na vita, na kurudi Misri;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati Farao alipowaachia Waisraeli waende zao, Mungu hakuwapitisha katika nchi ya Wafilisti, ingawa njia hiyo ilikuwa ya karibu. Mungu alisema, “Sipendi watu hawa wabadilishe nia na kurudi Misri wakijua itawabidi kupigana vita.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Farao alipowaachia watu waende, Mungu hakuwaongoza kufuata njia ipitiayo katika nchi ya Wafilisti, ingawa njia hiyo ilikuwa fupi zaidi. Kwa maana Mungu alisema, “Wakikabiliana na vita, wanaweza kubadili mawazo yao na kurudi Misri.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Farao alipowaachia watu waende, Mungu hakuwaongoza kufuata njia ipitiayo katika nchi ya Wafilisti, ingawa njia hiyo ilikuwa fupi zaidi. Kwa maana Mungu alisema, “Wakikabiliana na vita, wanaweza kubadili mawazo yao na kurudi Misri.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ilikuwa hapo Farao alipowaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakabadili nia watu hawa hapo watakapokumbana na vita, na kurudi Misri;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati Farao alipowaachia Waisraeli waende zao, Mungu hakuwapitisha katika nchi ya Wafilisti, ingawa njia hiyo ilikuwa ya karibu. Mungu alisema, “Sipendi watu hawa wabadilishe nia na kurudi Misri wakijua itawabidi kupigana vita.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Farao alipokwisha kuwapa hawa watu ruhusa kwenda zao, Mungu hakuwashikisha njia ya kupita katika nchi ya wafilisti iliyokuwa fupi, kwani Mungu alisema: Labda watu hawa watageuza miyo kwa kuona vita, warudi Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ilikuwa hapo Farao alipokwisha kuwaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakaghairi watu hawa hapo watakapokutana na vita, na kurudi Misri;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati mufalme wa Misri alipowaachilia Waisraeli wajiendee, Mungu hakuwapitisha katika inchi ya Wafilistini, ingawa njia hiyo ilikuwa ya karibu. Mungu alisema: “Sipendi watu hawa wabadilishe nia na kurudi Misri wakijua kama itawapasa kupigana vita.”