Exodus 13:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose akawaambia watu, “Ikumbukeni siku hii mliyotoka nchini Misri ambako mlikuwa watumwa. Hii ndiyo siku Mwenyezi-Mungu alipowatoa humo kwa mkono wake wenye nguvu. Katika siku hii, kamwe msile mkate uliotiwa chachu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Musa akawaambia watu, “Ikumbukeni siku hii, siku ambayo mlitoka katika nchi ya Misri, katika nchi ya utumwa, kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwatoa humo kwa mkono wenye nguvu. Msile chochote kilichotiwa chachu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa akawaambia hao watu, Kumbukeni siku hii, mliyotoka nchi ya Misri, kutoka nyumba ya utumwa; kwa kuwa Bwana aliwatoa mahali hapa kwa nguvu za mkono wake; na usiliwe mkate uliochachwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose akawaambia watu, “Ikumbukeni siku hii mliyotoka nchini Misri ambako mlikuwa watumwa. Hii ndiyo siku Mwenyezi-Mungu alipowatoa humo kwa mkono wake wenye nguvu. Katika siku hii, kamwe msile mkate uliotiwa chachu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Mose akawaambia watu, “Ikumbukeni siku hii, siku ambayo mlitoka katika nchi ya Misri, katika nchi ya utumwa, kwa sababu BWANA aliwatoa humo kwa mkono wenye nguvu. Msile cho chote kilichotiwa chachu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Musa akawaambia watu, “Ikumbukeni siku hii, siku ambayo mlitoka katika nchi ya Misri, katika nchi ya utumwa, kwa sababu bwana aliwatoa humo kwa mkono wenye nguvu. Msile chochote kilichotiwa chachu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa akawaambia hao watu, Kumbukeni siku hii, mliyotoka nchi ya Misri, kutoka nyumba ya utumwa; kwa kuwa BWANA aliwatoa mahali hapa kwa nguvu za mkono wake; na usiliwe mkate uliochachwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose akawaambia watu, “Ikumbukeni siku hii mliyotoka nchini Misri ambako mlikuwa watumwa. Hii ndiyo siku Mwenyezi-Mungu alipowatoa humo kwa mkono wake wenye nguvu. Katika siku hii, kamwe msile mkate uliotiwa chachu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mose akawaambia hao watu: Ikumbukeni siku hii ya leo kuwa ndiyo, mliyotoka huko Misri nyumbani, mlimokuwa watumwa! Kwani Bwana amewatoa huko kwa mkono wenye uwezo, siku hiyo kisiliwe cho chote chenye chachu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa akawaambia hao watu, Kumbukeni siku hii, mliyotoka nchi ya Misri, kutoka nyumba ya utumwa; kwa kuwa BWANA aliwatoa mahali hapa kwa nguvu za mkono wake; na usiliwe mkate uliochachwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa akawaambia watu: “Mukumbuke siku hii muliyotoka inchi ya Misri ambako mulikuwa watumwa. Hii ndiyo siku Yawe alipowatoa humo kwa mukono wake wenye nguvu. Katika siku hii, musikule mukate uliotiwa chachu.