Exodus 13:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na wakati Mwenyezi-Mungu atakapowafikisha katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Wahivi na Wayebusi, nchi ambayo aliwaapia babu zenu kwamba atawapa nyinyi, nchi inayotiririka maziwa na asali, ni lazima muiadhimishe sikukuu hii kila mwaka katika mwezi huu wa kwanza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu atakapokuleta katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Wahivi na Wayebusi, nchi aliyowaapia baba zako kukupa, nchi inayotiririka maziwa na asali, utaiadhimisha sikukuu hii katika mwezi huu:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Itakuwa hapo Bwana atakapowaleta mpaka nchi ya Wakanaani, na Wahiti, na Waamori, na Wahivi, na Wayebusi, nchi hiyo aliyowaapia baba zako kwamba atakupa wewe, ni nchi imiminikayo maziwa na asali, ndipo mtakapoushika utumishi huu katika mwezi huu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na wakati Mwenyezi-Mungu atakapowafikisha katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Wahivi na Wayebusi, nchi ambayo aliwaapia babu zenu kwamba atawapa nyinyi, nchi inayotiririka maziwa na asali, ni lazima muiadhimishe sikukuu hii kila mwaka katika mwezi huu wa kwanza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA atakapokuleta katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Wahivi na Wayebusi, nchi aliyowaapia baba zako kukupa, nchi itiririkayo maziwa na asali, utaiadhimisha sikukuu hii katika mwezi huu:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana atakapokuleta katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Wahivi na Wayebusi, nchi aliyowaapia baba zako kukupa, nchi itiririkayo maziwa na asali, utaiadhimisha sikukuu hii katika mwezi huu:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Itakuwa hapo BWANA atakapowaleta mpaka nchi ya Wakanaani, na Wahiti, na Waamori, na Wahivi, na Wayebusi, nchi hiyo aliyowaapia baba zako kwamba atakupa wewe, ni nchi imiminikayo maziwa na asali, ndipo mtakapoushika utumishi huu katika mwezi huu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na wakati Mwenyezi-Mungu atakapowafikisha katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Wahivi na Wayebusi, nchi ambayo aliwaapia babu zenu kwamba atawapa nyinyi, nchi inayotiririka maziwa na asali, ni lazima muiadhimishe sikukuu hii kila mwaka katika mwezi huu wa kwanza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Napo hapo, Bwana atakapokupeleka katika nchi yao Wakanaani na Wahiti na Waamori na Wahiwi na Wayebusi, aliyowaapia baba zako kukupa wewe, katika ile nchi ichuruzikayo maziwa na asali, huko shari uuangalie utumishi huu, uutumikie katika mwezi huu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Itakuwa hapo BWANA atakapowaleta mpaka nchi ya Wakanaani, na Wahiti, na Waamori, na Wahivi, na Wayebusi, nchi hiyo aliyowaapia baba zako kwamba atakupa wewe, ni nchi imiminikayo maziwa na asali, ndipo mtakapoushika utumishi huu katika mwezi huu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na wakati Yawe atakapowafikisha katika inchi ya Wakanana, Wahiti, Waamori, Wahivi, na Wayebusi, inchi ambayo aliwaapia babu zenu kwamba atawapa ninyi, inchi inayotiririka maziwa na asali, munapaswa kushika sikukuu hii kila mwaka katika mwezi huu wa kwanza.