Exodus 14:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli walipotazama na kumwona Farao akija na jeshi lake dhidi yao, walishikwa na hofu kubwa, wakamlilia Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Farao alipokaribia, Waisraeli wakainua macho yao, wakawaona Wamisri wakija nyuma yao. Wakashikwa na hofu, wakamlilia Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli wakainua macho yao, na tazama, Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli walipotazama na kumwona Farao akija na jeshi lake dhidi yao, walishikwa na hofu kubwa, wakamlilia Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Farao alipokaribia, Waisraeli wakainua macho yao, wakawaona Wamisri wakija nyuma yao. Wakashikwa na hofu, wakamlilia BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Farao alipokaribia, Waisraeli wakainua macho yao, wakawaona Wamisri wakija nyuma yao. Wakashikwa na hofu, wakamlilia bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli walipoangalia nyuma na kuona Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waisraeli walipotazama na kumwona Farao akija na jeshi lake dhidi yao, walishikwa na hofu kubwa, wakamlilia Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Farao alipofika karibu, wana wa Isiraeli wakayainua macho yao, wakawaona Wamisri, walivyofuata nyuma; ndipo, waliposhikwa na woga kabisa, wakampigia Bwana makelele wao wana wa Isiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli wakainua macho yao, na tazama, Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waisraeli walipoinua macho na kumwona mufalme wa Misri akikuja na jeshi lake nyuma yao, wakashikwa na hofu kubwa, wakamulilia Yawe.