Exodus 14:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose akaunyosha mkono wake juu ya bahari, naye Mwenyezi-Mungu akaisukuma bahari nyuma kwa upepo mkali toka mashariki. Upepo huo ulivuma usiku kucha, ukaigawa bahari sehemu mbili na katikati kukatokeza nchi kavu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Musa akanyoosha mkono wake juu ya bahari, naye Mwenyezi Mungu akayasukuma maji ya bahari nyuma kwa upepo mkali wa mashariki usiku ule wote na kupafanya nchi kavu. Maji yakagawanyika,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa; akanyosha mkono wake juu ya bahari; Bwana akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu, maji yakagawanyika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose akaunyosha mkono wake juu ya bahari, naye Mwenyezi-Mungu akaisukuma bahari nyuma kwa upepo mkali toka mashariki. Upepo huo ulivuma usiku kucha, ukaigawa bahari sehemu mbili na katikati kukatokeza nchi kavu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Mose akanyosha mkono wake juu ya bahari, naye BWANA akayasukuma maji ya bahari nyuma kwa upepo mkali wa mashariki usiku ule wote na kupafanya nchi kavu. Maji yakagawanyika,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Musa akanyoosha mkono wake juu ya bahari, naye bwana akayasukuma maji ya bahari nyuma kwa upepo mkali wa mashariki usiku ule wote na kupafanya nchi kavu. Maji yakagawanyika,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa; akanyosha mkono wake juu ya bahari; BWANA akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu, maji yakagawanyika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose akaunyosha mkono wake juu ya bahari, naye Mwenyezi-Mungu akaisukuma bahari nyuma kwa upepo mkali toka mashariki. Upepo huo ulivuma usiku kucha, ukaigawa bahari sehemu mbili na katikati kukatokeza nchi kavu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mose alipoikunjulia bahari mkono wake, Bwana akaiendesha bahari kwa nguvu ya upepo uliotoka upande wa maawioni kwa jua na kuvuma kabisa usiku wote, akaipwelesha bahari kuwa pakavu, maji yakigawanyika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa; akanyosha mkono wake juu ya bahari; BWANA akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu, maji yakagawanyika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa akanyoosha mukono wake juu ya bahari, naye Yawe akasukuma bahari nyuma kwa upepo mukali toka upande wa mashariki. Upepo ule ulivuma usiku kucha, ukagawanya bahari sehemu mbili na katikati kukatokea inchi kavu.