Exodus 14:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi na kuwafunika Wamisri pamoja na magari yao na wapandafarasi wao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Nyoosha mkono wako juu ya bahari ili maji yarudi yawafunike Wamisri, magari yao ya vita, na wapanda farasi wao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi na kuwafunika Wamisri pamoja na magari yao na wapandafarasi wao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo BWANA akamwambia Mose, “Nyosha mkono wako juu ya bahari ili maji yarudiane yawafunike Wamisri, magari yao ya vita na wapanda farasi wao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo bwana akamwambia Musa, “Nyoosha mkono wako juu ya bahari ili maji yarudiane yawafunike Wamisri, magari yao ya vita na wapanda farasi wao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi na kuwafunika Wamisri pamoja na magari yao na wapandafarasi wao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Bwana akamwambia Mose: Ikunjulie bahari mkono wako, maji yarudiane na kuwatosa Wamisri na magari yao pamoja nao walioyapanda!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yawe akamwambia Musa: “Nyoosha mukono wako juu ya bahari, kusudi maji yarudie na kuwafunika Wamisri pamoja na magari yao na wapanda-farasi wao.”