Exodus 14:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Mose akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka bahari ikarudia hali yake ilivyokuwa. Wamisri wakajaribu kuyakimbia maji lakini Mwenyezi-Mungu akawasukumizia baharini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa akanyoosha mkono wake juu ya bahari, kulipopambazuka bahari ikarudi mahali pake. Wamisri wakajaribu kuyakimbia maji, lakini Mwenyezi Mungu akawasukumia ndani ya bahari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake; na Bwana akawakukutia mbali hao Wamisri kati ya bahari.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Mose akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka bahari ikarudia hali yake ilivyokuwa. Wamisri wakajaribu kuyakimbia maji lakini Mwenyezi-Mungu akawasukumizia baharini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose akanyosha mkono wake juu ya bahari, wakati wa mapambazuko bahari ikarudiana na kuwa kama kawaida. Wamisri wakajaribu kuyakimbia maji, lakini BWANA akawasukumia ndani ya bahari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa akanyoosha mkono wake juu ya bahari, wakati wa mapambazuko bahari ikarudiana na kuwa kama kawaida. Wamisri wakajaribu kuyakimbia maji, lakini bwana akawasukumia ndani ya bahari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakajaribu kuyakimbia maji na BWANA akawaangamiza hao Wamisri katika bahari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Mose akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka bahari ikarudia hali yake ilivyokuwa. Wamisri wakajaribu kuyakimbia maji lakini Mwenyezi-Mungu akawasukumizia baharini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mose alipoikunjulia bahari mkono wake, ndipo, maji ya bahari yalipourudia mwendo wake wa siku zote, nayo yalifanyika, kulipopambazuka. Nao Wamisri walipokimbia wakapatwa nayo; ndivyo, Bwana alivyowakumba Wamisri kuingia katikati ya bahari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake; na BWANA akawakukutia mbali hao Wamisri kati ya bahari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Musa akanyoosha mukono wake juu ya bahari na kulipopambazuka bahari ikarudilia hali yake ilivyokuwa. Wamisri wakajaribu kukimbia maji lakini Yawe akawasukumizia ndani ya bahari.