Exodus 14:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo mimi nitamfanya Farao kuwa mkaidi, naye atawafuatia. Nami nitajipatia utukufu kwa kumwangamiza yeye na jeshi lake. Hapo Wamisri watatambua kwamba mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.” Basi, Waisraeli wakafanya hivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nami nitaufanya moyo wa Farao mgumu, naye atawafuatilia. Lakini nitajipatia utukufu kwa ajili yangu mwenyewe kupitia Farao na jeshi lake lote, nao Wamisri watajua kuwa mimi ndimi Mwenyezi Mungu.” Kwa hiyo Waisraeli wakafanya hivyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitaufanya uwe mgumu moyo wa Farao, naye atafuata nyuma yao; nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote; na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Basi wakafanya hivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo mimi nitamfanya Farao kuwa mkaidi, naye atawafuatia. Nami nitajipatia utukufu kwa kumwangamiza yeye na jeshi lake. Hapo Wamisri watatambua kwamba mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.” Basi, Waisraeli wakafanya hivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nami nitaufanya moyo wa Farao mgumu, naye atawafuatilia. Lakini nitajipatia utukufu kwa ajili yangu mwenyewe kupitia Farao na jeshi lake lote, nao Wamisri watajua kuwa mimi ndimi BWANA.” Kwa hiyo Waisraeli wakafanya hivyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nami nitaufanya moyo wa Farao mgumu, naye atawafuatilia. Lakini nitajipatia utukufu kwa ajili yangu mwenyewe kupitia Farao na jeshi lake lote, nao Wamisri watajua kuwa mimi ndimi bwana.” Kwa hiyo Waisraeli wakafanya hivyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitaufanya uwe mgumu moyo wa Farao, naye atafuata nyuma yao; nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote; na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Basi wakafanya hivyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo mimi nitamfanya Farao kuwa mkaidi, naye atawafuatia. Nami nitajipatia utukufu kwa kumwangamiza yeye na jeshi lake. Hapo Wamisri watatambua kwamba mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.” Basi, Waisraeli wakafanya hivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami nitaushupaza moyo wa Farao, ajihimize kuwafuata, nijipatie utukufu kwake Farao na kwa vikosi vyake vyote, Wamisri watambue, ya kuwa mimi ni Bwana. Basi, wakafanya hivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitaufanya uwe mgumu moyo wa Farao, naye atafuata nyuma yao; nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote; na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Basi wakafanya hivyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu mimi nitafanya moyo wa mufalme wa Misri kuwa mugumu, naye atawafuatilia. Nami nitajipatia utukufu kwa kumwangamiza yeye na jeshi lake. Halafu Wamisri watatambua kwamba mimi ni Yawe.” Basi, Waisraeli wakafanya hivyo.