Exodus 14:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu akamfanya Farao, mfalme wa Misri, kuwa mkaidi naye akawafuatia Waisraeli ambao walikuwa wameondoka Misri kwa ushupavu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu akaufanya moyo wa Farao mfalme wa Misri kuwa mgumu, kwa hiyo akawafuatia Waisraeli, waliokuwa wakiondoka Misri kwa ujasiri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Bwana akaufanya moyo wake Farao mfalme wa Misri kuwa mgumu, naye akawafuata wana wa Israeli; kwa sababu wana wa Israeli walitoka kwa ujeuri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu akamfanya Farao, mfalme wa Misri, kuwa mkaidi naye akawafuatia Waisraeli ambao walikuwa wameondoka Misri kwa ushupavu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA akaufanya mgumu moyo wa Farao, mfalme wa Misri, kwa hiyo akawafuatia Waisraeli, waliokuwa wakiondoka Misri kwa ujasiri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana akaufanya mgumu moyo wa Farao, mfalme wa Misri, kwa hiyo akawafuatia Waisraeli, waliokuwa wakiondoka Misri kwa ujasiri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na BWANA akaufanya moyo wake Farao mfalme wa Misri kuwa mgumu, naye akawafuata wana wa Israeli; kwa sababu wana wa Israeli walitoka kwa jeuri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu akamfanya Farao, mfalme wa Misri, kuwa mkaidi naye akawafuatia Waisraeli ambao walikuwa wameondoka Misri kwa ushupavu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maana Bwana alikuwa ameushupaza moyo wake Farao, mfalme wa Misri, ajihimize kuwafuata wana wa Isiraeli, ijapo Waisiraeli walitoka kwa nguvu za mkono ulioko juu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na BWANA akaufanya moyo wake Farao mfalme wa Misri kuwa mgumu, naye akawafuata wana wa Israeli; kwa sababu wana wa Israeli walitoka kwa ujeuri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akafanya moyo wa mufalme wa Misri kuwa mugumu, naye akawafuatilia Waisraeli ambao walikuwa wameondoka Misri katika uhuru.