Exodus 15:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ewe Mwenyezi-Mungu, ni nani kati ya miungu anayelingana nawe? Ni nani aliye kama wewe uliye mtakatifu mkuu, utishaye kwa matendo matukufu, unayetenda mambo ya ajabu?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni nani miongoni mwa miungu aliye kama wewe, Ee Mwenyezi Mungu? Ni nani kama Wewe: uliyetukuka katika utakatifu, utishaye katika utukufu, ukitenda maajabu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Bwana, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ewe Mwenyezi-Mungu, ni nani kati ya miungu anayelingana nawe? Ni nani aliye kama wewe uliye mtakatifu mkuu, utishaye kwa matendo matukufu, unayetenda mambo ya ajabu?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ni nani miongoni mwa miungu aliye kama wewe, Ee BWANA? Ni nani kama Wewe: uliyetukuka katika utakatifu, utishaye katika utukufu, ukitenda maajabu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ni nani miongoni mwa miungu aliye kama wewe, Ee bwana? Ni nani kama Wewe: uliyetukuka katika utakatifu, utishaye katika utukufu, ukitenda maajabu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee BWANA, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ewe Mwenyezi-Mungu, ni nani kati ya miungu anayelingana nawe? Ni nani aliye kama wewe uliye mtakatifu mkuu, utishaye kwa matendo matukufu, unayetenda mambo ya ajabu?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Miongoni mwa miungu yuko nani anayefanana na wewe, Bwana? Yuko nani anayefanana na wewe kwa utukufu na kwa utakatifu? Anayetisha kwa matendo yanayoshangiliwa, naye akifanya vioja?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee BWANA, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ewe Yawe, ni nani kati ya miungu anayelingana nawe? Ni nani aliyekuwa kama wewe unayekuwa mutakatifu mukubwa, unayetisha kwa matendo matukufu, unayetenda mambo ya ajabu?