Exodus 15:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati farasi wa Farao na magari yake pamoja na wapandafarasi wake walipoingia mahali pakavu baharini, Mwenyezi-Mungu aliyarudisha maji ya bahari yakawafunika. Lakini Waisraeli waliendelea kutembea pakavu katikati ya bahari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Farasi wa Farao, magari yake ya vita na wapanda farasi wake walipoingia baharini, Mwenyezi Mungu aliyarudisha maji ya bahari yakawafunika, lakini Waisraeli walipita baharini mahali pakavu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana farasi za Farao na magari yake na wapanda farasi wake waliingia ndani ya bahari, Bwana akayarudisha maji ya bahari juu yao; bali wana wa Israeli walikwenda katika nchi kavu katikati ya bahari.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati farasi wa Farao na magari yake pamoja na wapandafarasi wake walipoingia mahali pakavu baharini, Mwenyezi-Mungu aliyarudisha maji ya bahari yakawafunika. Lakini Waisraeli waliendelea kutembea pakavu katikati ya bahari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Farasi wa Farao, magari yake ya vita na wapanda farasi wake walipoingia baharini, BWANA aliyarudisha maji ya bahari yakawafunika, lakini wana wa Israeli walipita baharini mahali pakavu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Farasi wa Farao, magari yake ya vita na wapanda farasi wake walipoingia baharini, bwana aliyarudisha maji ya bahari yakawafunika, lakini wana wa Israeli walipita baharini mahali pakavu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana farasi wa Farao na magari yake na wapanda farasi wake waliingia ndani ya bahari, BWANA akayarudisha maji ya bahari juu yao; bali wana wa Israeli walikwenda katika nchi kavu katikati ya bahari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati farasi wa Farao na magari yake pamoja na wapandafarasi wake walipoingia mahali pakavu baharini, Mwenyezi-Mungu aliyarudisha maji ya bahari yakawafunika. Lakini Waisraeli waliendelea kutembea pakavu katikati ya bahari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani farasi wa Farao na magari yake pamoja nao walioyapanda walipoingia baharini, Bwana akayarudisha maji ya bahari juu yao, wana wa Isiraeli walipokwisha kupita pakavu katikati ya bahari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana farasi za Farao na magari yake na wapanda farasi wake waliingia ndani ya bahari, BWANA akayarudisha maji ya bahari juu yao; bali wana wa Israeli walikwenda katika nchi kavu katikati ya bahari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati farasi wa mufalme wa Misri na magari yake pamoja na wapanda-farasi wake walipoingia pahali pakavu katika bahari, Yawe aliyarudisha maji ya bahari yakawafunika. Lakini Waisraeli waliendelea kutembea pakavu katikati ya bahari.