Exodus 15:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Mose akamlilia Mwenyezi-Mungu, naye akamwonesha kipande cha mti, na Mose akakitumbukiza katika maji; maji hayo yakawa mazuri. Huko Mungu aliwapa Waisraeli amri na agizo, ili ajue uthabiti wao,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Musa akamlilia Mwenyezi Mungu, naye Mwenyezi Mungu akamwonesha kipande cha mti. Akakitupa ndani ya maji, nayo maji yakawa matamu. Huko Mwenyezi Mungu akawapa amri na sheria na huko akawajaribu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akamlilia Bwana; Bwana akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawaonja huko;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Mose akamlilia Mwenyezi-Mungu, naye akamwonesha kipande cha mti, na Mose akakitumbukiza katika maji; maji hayo yakawa mazuri. Huko Mungu aliwapa Waisraeli amri na agizo, ili ajue uthabiti wao,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Mose akamlilia BWANA, naye BWANA akamwonyesha kipande cha mti. Akakitupa ndani ya maji, nayo maji yakawa matamu. Huko BWANA akawapa amri na sheria na huko akawajaribu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Musa akamlilia bwana, naye bwana akamwonyesha kipande cha mti. Akakitupa ndani ya maji, nayo maji yakawa matamu. Huko bwana akawapa amri na sheria na huko akawajaribu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akamlilia BWANA; BWANA akamwonesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawajaribu huko;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Mose akamlilia Mwenyezi-Mungu, naye akamwonesha kipande cha mti, na Mose akakitumbukiza katika maji; maji hayo yakawa mazuri. Huko Mungu aliwapa Waisraeli amri na agizo, ili ajue uthabiti wao,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye alipomlilia Bwana, Bwana akamwonyesha mti; alipoutupa mti huo majini, maji yakawa matamu. Hapo Bwana akawatolea maongozi yapasayo, akawajaribu hapo
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akamlilia BWANA; BWANA akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawaonja huko;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Musa akamulilia Yawe, naye akamwonyesha kipande cha muti, na Musa akakitumbukiza katika maji. Maji hayo yakakuwa mazuri. Kule Mungu aliwapa Waisraeli sharti na agizo, kusudi awapime,