Exodus 15:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akawaambia, “Ikiwa mtaisikiliza kwa makini sauti yangu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kutenda yaliyo sawa mbele yangu, na kuheshimu amri na maagizo yangu yote, basi, mimi sitawaletea yale magonjwa niliyowaletea Wamisri. Kwa sababu, mimi ndimi Mwenyezi-Mungu ninayewaponya nyinyi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu akasema, “Mkisikiliza kwa makini sauti ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na kuyafanya yaliyo mema machoni pake, na mkiyatii maagizo yake na kuzishika amri zake zote, sitaleta juu yenu ugonjwa wowote niliowaletea Wamisri, kwa kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, niwaponyaye.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akawaambia, “Ikiwa mtaisikiliza kwa makini sauti yangu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kutenda yaliyo sawa mbele yangu, na kuheshimu amri na maagizo yangu yote, basi, mimi sitawaletea yale magonjwa niliyowaletea Wamisri. Kwa sababu, mimi ndimi Mwenyezi-Mungu ninayewaponya nyinyi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu akasema, “Kama mkisikiliza kwa bidii sauti ya BWANA Mungu wenu na kuyafanya yaliyo sawa machoni pake, kama mkiyatii maagizo yake na kuzishika amri zake zote, sitaleta juu yenu ugonjwa wo wote niliowaletea Wamisri, kwa kuwa Mimi ndimi BWANA, niwaponyaye.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mungu akasema, “Kama mkisikiliza kwa bidii sauti ya bwana Mwenyezi Mungu wenu na kuyafanya yaliyo sawa machoni pake, kama mkiyatii maagizo yake na kuzishika amri zake zote, sitaleta juu yenu ugonjwa wowote niliowaletea Wamisri, kwa kuwa Mimi ndimi bwana, niwaponyaye.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akawaambia, Kwamba utaisikiliza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yoyote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akawaambia, “Ikiwa mtaisikiliza kwa makini sauti yangu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kutenda yaliyo sawa mbele yangu, na kuheshimu amri na maagizo yangu yote, basi, mimi sitawaletea yale magonjwa niliyowaletea Wamisri. Kwa sababu, mimi ndimi Mwenyezi-Mungu ninayewaponya nyinyi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akiwaambia: Kama utaisikia sauti ya Bwana Mungu wako na kuyafanya yanyokayo machoni pake na kuyategea maagizo yake masiko yako na kuyaangalia maongozi yake yote, ndipo, utakapoona, ya kuwa sikutii yale magonjwa yote, niliyowatia Wamisri, kwani mimi Bwana ni mponya wako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
akawaambia: “Ikiwa mutaisikiliza kwa uaminifu sauti yangu mimi Yawe, Mungu wenu, kutenda yale yanayokuwa sawa mbele yangu, na kuheshimu amri na masharti yangu yote, basi, mimi sitawaletea yale magonjwa niliyowaletea Wamisri. Kwa sababu, mimi ni Yawe ninayewaponya ninyi.”