Exodus 15:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Adui alijisemea, ‘Nitawafuata na kuwakamata; nitagawanya nyara mpaka hamu yangu iishe. Tutaufuta upanga wetu, tutawaangamiza kwa mkono wetu.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Adui alijivuna, ‘Nitawafuatia, nitawapata. Nitagawanya nyara; nitajishibisha kwao. Nitafuta upanga wangu na mkono wangu utawaangamiza.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Adui akasema, Nitafuatia, nitapata, nitagawanya nyara, Nafsi yangu itashibishwa na wao; Nitaufuta upanga wangu, mkono wangu utawaangamiza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Adui alijisemea, ‘Nitawafuata na kuwakamata; nitagawanya nyara mpaka hamu yangu iishe. Tutaufuta upanga wetu, tutawaangamiza kwa mkono wetu.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Adui alijivuna, ‘Nitawafuatia, nitawapata. Nitagawanya nyara; nitajishibisha kwa wao. Nitafuta upanga wangu na mkono wangu utawaangamiza.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Adui alijivuna, ‘Nitawafuatia, nitawapata. Nitagawanya nyara; nitajishibisha kwa wao. Nitafuta upanga wangu na mkono wangu utawaangamiza.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Adui akasema, Nitafuata, nitapata, nitagawanya nyara, Nafsi yangu itashibishwa na wao; Nitaufuta upanga wangu, mkono wangu utawaangamiza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Adui alijisemea, ‘Nitawafuata na kuwakamata; nitagawanya nyara mpaka hamu yangu iishe. Tutaufuta upanga wetu, tutawaangamiza kwa mkono wetu.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Adui aliposema: Nijihimize kufuata! Nitafika, roho yangu itapata kushiba, nikigawanya nyara; nitauchomoa upanga wangu, mkono wangu uwaangamize:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Adui akasema, Nitafuatia, nitapata, nitagawanya nyara, Nafsi yangu itashibishwa na wao; Nitaufuta upanga wangu, mkono wangu utawaangamiza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Adui akajisemesha: ‘Nitawafuata na kuwakamata; nitagawanya vitu mpaka hamu yangu iishe. Tutafuta upanga wetu, tutawaangamiza kwa mukono wetu.’