Exodus 16:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wote walipokipima kipimo walichookota katika pishi, waligundua kuwa aliyeokota kingi hakuwa na cha ziada, na aliyeokota kidogo, hakupungukiwa. Kila mmoja alikuwa ameokota kiasi alichoweza kula.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao walipopima katika pishi, yule aliyekusanya zaidi hakuwa na ziada, wala aliyekusanya kidogo hakupungukiwa. Kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao walipoipima kwa pishi, yeye aliyekuwa ameokota kingi hakubakiwa na kitu, na yeye aliyekuwa ameokota kichache hakupungukiwa; wakaokota kila mtu kama ulaji wake ulivyokuwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wote walipokipima kipimo walichookota katika pishi, waligundua kuwa aliyeokota kingi hakuwa na cha ziada, na aliyeokota kidogo, hakupungukiwa. Kila mmoja alikuwa ameokota kiasi alichoweza kula.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao walipopima katika pishi, yule aliyekusanya zaidi hakuwa na ziada, pia yule aliyekusanya kidogo hakuwa na upungufu. Kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao walipopima katika pishi, yule aliyekusanya zaidi hakuwa na ziada, wala aliyekusanya kidogo hakupungukiwa. Kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao walipoipima kwa pishi, yeye aliyekuwa ameokota kingi hakubakiwa na kitu, na yeye aliyekuwa ameokota kichache hakupungukiwa; wakaokota kila mtu kama ulaji wake ulivyokuwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wote walipokipima kipimo walichookota katika pishi, waligundua kuwa aliyeokota kingi hakuwa na cha ziada, na aliyeokota kidogo, hakupungukiwa. Kila mmoja alikuwa ameokota kiasi alichoweza kula.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
lakini walipopima kwa pishi, yule aliyeokota nyingi hakufurikiwa, wala aliyeokota chache hakupungukiwa, ila walikuwa wameokota kila mtu zilizompasa za kula.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao walipoipima kwa pishi, yeye aliyekuwa ameokota kingi hakubakiwa na kitu, na yeye aliyekuwa ameokota kichache hakupungukiwa; wakaokota kila mtu kama ulaji wake ulivyokuwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wote walipopima kiasi walichookota katika kipimo cha litre ine, walitambua kwamba aliyeokota kingi hakukuwa na cha zaidi na aliyeokota kidogo, hakupungukiwa. Kila mumoja alikuwa ameokota kiasi alichoweza kula.