Exodus 16:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini watu hawakumsikiliza Mose. Baadhi yao walijibakizia chakula mpaka asubuhi. Lakini asubuhi chakula hicho kikawa kimeoza na kuwa na mabuu. Mose akawakasirikia sana watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo, wengine hawakuzingatia aliyosema Musa, wakahifadhi kiasi fulani hadi asubuhi, lakini kile alichohifadhi kikajaa mabuu na kuanza kunuka. Kwa hiyo Musa akawakasirikia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini hawakumsikiza Musa; wengine miongoni mwao wakakisaza hata asubuhi, nacho kikaingia mabuu na kutoa uvundo; Musa akawakasirikia sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini watu hawakumsikiliza Mose. Baadhi yao walijibakizia chakula mpaka asubuhi. Lakini asubuhi chakula hicho kikawa kimeoza na kuwa na mabuu. Mose akawakasirikia sana watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo, wengine hawakuzingatia aliyosema Mose, wakahifadhi kiasi fulani mpaka asubuhi, lakini kile alichohifadhi kikajaa mabuu na kuanza kunuka. Kwa hiyo Mose akawakasirikia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo, wengine hawakuzingatia aliyosema Musa, wakahifadhi kiasi fulani mpaka asubuhi, lakini kile alichohifadhi kikajaa mabuu na kuanza kunuka. Kwa hiyo Musa akawakasirikia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini hawakumsikiliza Musa; wengine miongoni mwao wakakisaza hata asubuhi, nacho kikaingia mabuu na kutoa uvundo; Musa akawakasirikia sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini watu hawakumsikiliza Mose. Baadhi yao walijibakizia chakula mpaka asubuhi. Lakini asubuhi chakula hicho kikawa kimeoza na kuwa na mabuu. Mose akawakasirikia sana watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hawakumsikia Mose, wengine wakasaza za kesho, zikapata funyo ndani, zikanuka vibaya. Naye Mose akawakasirikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini hawakumsikiza Musa; wengine miongoni mwao wakakisaza hata asubuhi, nacho kikaingia mabuu na kutoa uvundo; Musa akawakasirikia sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini watu hawakumusikiliza Musa. Wamoja kati yao walijiwekea chakula mpaka asubui. Lakini asubui chakula hicho kikakuwa kimeoza na kuwa na vidudu. Musa akawakasirikia sana watu.