Exodus 16:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika siku ya sita, Waisraeli walikusanya chakula hicho maradufu, pishi nne kwa kila mtu. Basi, wazee wote wa jumuiya ya Waisraeli walimwendea Mose, wakamweleza jambo hilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya sita, wakakusanya mara mbili, kiasi cha pishi mbili kwa kila mtu, nao viongozi wa jumuiya wakaja kumwarifu Musa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ikawa siku ya sita wakaokota kile chakula sehemu maradufu, kila mtu pishi mbili; na wazee wote wa mkutano wakaenda na kumwambia Musa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika siku ya sita, Waisraeli walikusanya chakula hicho maradufu, pishi nne kwa kila mtu. Basi, wazee wote wa jumuiya ya Waisraeli walimwendea Mose, wakamweleza jambo hilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ya sita, wakakusanya mara mbili, kiasi cha pishi mbili kwa kila mtu, nao viongozi wa jumuiya wakaja kumwuarifu Mose.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ya sita, wakakusanya mara mbili, kiasi cha pishi mbili kwa kila mtu, nao viongozi wa jumuiya wakaja kumwarifu Musa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi ikawa siku ya sita wakaokota kile chakula sehemu maradufu, kila mtu pishi mbili; na wazee wote wa mkutano wakaenda na kumwambia Musa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika siku ya sita, Waisraeli walikusanya chakula hicho maradufu, pishi nne kwa kila mtu. Basi, wazee wote wa jumuiya ya Waisraeli walimwendea Mose, wakamweleza jambo hilo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini walipookota siku ya sita, hivyo vilaji vilikuwa kipimo cha siku zote mara mbili, vibaba vinne mtu mmoja. Ndipo, wakuu wote wa mkutano walipokwenda kwa Mose kumpasha habari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ikawa siku ya sita wakaokota kile chakula sehemu maradufu, kila mtu pishi mbili; na wazee wote wa mkutano wakaenda na kumwambia Musa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku ya sita, Waisraeli walikusanya chakula hicho mara mbili, vipimo viwili vya litre ine kwa kila mutu. Basi, wazee wote wa Waisraeli wakamwendea Musa, wakamwelezea jambo hilo.