Exodus 16:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose akawaambia, “Hii ndiyo amri ya Mwenyezi-Mungu. Kesho ni siku rasmi ya mapumziko; ni Sabato takatifu ya Mwenyezi-Mungu. Basi, nendeni mkapike au mkachemshe kile chakula mnachohitaji leo, na chakula kitakachosalia kiwekeni mpaka kesho.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa akawaambia, “Hivi ndivyo alivyoagiza Mwenyezi Mungu: ‘Kesho itakuwa Sabato ya mapumziko, Sabato takatifu kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo okeni kile mnachotaka kuoka na mchemshe kile mnachotaka kuchemsha. Hifadhini chochote kinachobaki na mkiweke hadi asubuhi.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia, Ndilo neno alilonena Bwana Kesho ni starehe takatifu, Sabato takatifu kwa Bwana; okeni mtakachooka, na kutokosa mtakachotokosa; na hicho kitakachowasalia jiwekeeni kilindwe hata asubuhi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose akawaambia, “Hii ndiyo amri ya Mwenyezi-Mungu. Kesho ni siku rasmi ya mapumziko; ni Sabato takatifu ya Mwenyezi-Mungu. Basi, nendeni mkapike au mkachemshe kile chakula mnachohitaji leo, na chakula kitakachosalia kiwekeni mpaka kesho.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose akawaambia, “Hivi ndivyo alivyoagiza BWANA: ‘Kesho itakuwa siku ya mapumziko, Sabato takatifu kwa BWANA. Kwa hiyo okeni kile mnachotaka kuoka na mchemshe kile mnachotaka kuchemsha. Hifadhini cho chote kinachobaki na mkiweke mpaka asubuhi.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa akawaambia, “Hivi ndivyo alivyoagiza bwana: ‘Kesho itakuwa siku ya mapumziko, Sabato takatifu kwa bwana. Kwa hiyo okeni kile mnachotaka kuoka na mchemshe kile mnachotaka kuchemsha. Hifadhini chochote kinachobaki na mkiweke mpaka asubuhi.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia, Ndilo neno alilonena BWANA Kesho ni starehe takatifu, Sabato takatifu kwa BWANA; okeni mtakachooka, na kutokosa mtakachotokosa; na hicho kitakachowasalia jiwekeeni kilindwe hata asubuhi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose akawaambia, “Hii ndiyo amri ya Mwenyezi-Mungu. Kesho ni siku rasmi ya mapumziko; ni Sabato takatifu ya Mwenyezi-Mungu. Basi, nendeni mkapike au mkachemshe kile chakula mnachohitaji leo, na chakula kitakachosalia kiwekeni mpaka kesho.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akawaambia: Hili ndilo, Bwana alilolisema kwamba: Kesho ni siku takatifu ya mapumziko ya kumpumzikia Bwana. Mnazotaka kuzikaanga zikaangeni! Mnazotaka kuzipika zipikeni! Zitakazosalia jiwekeeni za kungoja kesho!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia, Ndilo neno alilonena BWANA Kesho ni starehe takatifu, Sabato takatifu kwa BWANA; okeni mtakachooka, na kutokosa mtakachotokosa; na hicho kitakachowasalia jiwekeeni kilindwe hata asubuhi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa akawaambia: “Hii ndiyo amri ya Yawe. Kesho ni siku ya mapumziko. Ni Sabato takatifu ya Yawe. Basi, muende mupike au kuchemusha kile chakula munachohitaji leo na chakula kitakachobakia mukiweke mpaka kesho.”