Exodus 16:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena Mose akasema, “Jioni, Mwenyezi-Mungu atawapeni nyama mle, na asubuhi atawapeni mikate mle mshibe, maana yeye ameyasikia manunguniko mliyomnungunikia. Sisi ni nani hata mtunungunikie? Msitunungunikie sisi bali mnungunikieni Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Musa akasema, “Mtajua kuwa alikuwa Mwenyezi Mungu wakati atakapowapa nyama mle ifikapo jioni na mikate yote mtakayohitaji asubuhi kwa sababu amesikia manung’uniko yenu dhidi yake. Sisi ni nani? Hamnung’uniki dhidi yetu, bali dhidi ya Mwenyezi Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa akasema, Ndilo litakalokuwa, hapo Bwana atakapowapa nyama wakati wa jioni mle, na asubuhi mikate hata mkakinai; kwa kuwa Bwana asikia manung'uniko yenu mliyomnung'unikia yeye; na sisi tu nani? Manung'uniko yenu hayakuwa juu yetu sisi, ila juu ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena Mose akasema, “Jioni, Mwenyezi-Mungu atawapeni nyama mle, na asubuhi atawapeni mikate mle mshibe, maana yeye ameyasikia manung'uniko mliyomnung'unikia. Sisi ni nani hata mtunung'unikie? Msitunung'unikie sisi bali mnung'unikieni Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia Mose akasema, “Mtajua kuwa alikuwa BWANA wakati atakapowapa nyama mle ifikapo jioni na mikate yote mtakayohitaji asubuhi kwa sababu amesikia manung'uniko yenu dhidi yake. Sisi ni nani? Hamnung'uniki dhidi yetu, bali dhidi ya BWANA.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia Musa akasema, “Mtajua kuwa alikuwa bwana wakati atakapowapa nyama mle ifikapo jioni na mikate yote mtakayohitaji asubuhi kwa sababu amesikia manung’uniko yenu dhidi yake. Sisi ni nani? Hamnung’uniki dhidi yetu, bali dhidi ya bwana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa akasema, Ndilo litakalokuwa, hapo BWANA atakapowapa nyama wakati wa jioni mle, na asubuhi mikate hata mkakinai; kwa kuwa BWANA asikia manung'uniko yenu mliyomnung'unikia yeye; na sisi tu nani? Manung'uniko yenu hayakuwa juu yetu sisi, ila juu ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena Mose akasema, “Jioni, Mwenyezi-Mungu atawapeni nyama mle, na asubuhi atawapeni mikate mle mshibe, maana yeye ameyasikia manunguniko mliyomnungunikia. Sisi ni nani hata mtunungunikie? Msitunungunikie sisi bali mnungunikieni Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena Mose akawaambia: Mtamjua Bwana hapo, atakapowapa leo jioni nyama za kula, tena asubuhi mikate ya kushiba, kwani Bwana amesikia, mlivyomnung'unikia yeye, maana sisi tu watu gani? Hamkutunung'unikia sisi, ila Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa akasema, Ndilo litakalokuwa, hapo BWANA atakapowapa nyama wakati wa jioni mle, na asubuhi mikate hata mkakinai; kwa kuwa BWANA asikia manung’uniko yenu mliyomnung’unikia yeye; na sisi tu nani? Manung’uniko yenu hayakuwa juu yetu sisi, ila juu ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena Musa akasema: “Magaribi, Yawe atawapa nyama mupate kula na asubui atawapa mikate mupate kula na kushiba. Maana yeye ameyasikia manunguniko muliyomunungunikia. Sisi ni nani hata mutunungunikie? Musitunungunikie sisi lakini mumunungunikie Yawe.”