Exodus 17:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kutoka jangwa la Sini, jumuiya yote ya Waisraeli ilisafiri hatua kwa hatua kama alivyoamuru Mwenyezi-Mungu, watu wakapiga kambi huko Refidimu. Lakini huko hakukuwa na maji ya kunywa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jumuiya yote ya Israeli ikaondoka kutoka Jangwa la Sini, ikisafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kama Mwenyezi Mungu alivyoagiza. Wakapiga kambi huko Refidimu, lakini hapakuwa na maji ya watu kunywa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mkutano wote wa wana wa Israeli ukasafiri, kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama Bwana alivyowaagiza, wakatua Refidimu; napo hapakuwa na maji, watu wanywe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kutoka jangwa la Sini, jumuiya yote ya Waisraeli ilisafiri hatua kwa hatua kama alivyoamuru Mwenyezi-Mungu, watu wakapiga kambi huko Refidimu. Lakini huko hakukuwa na maji ya kunywa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jumuiya yote ya Israeli ikaondoka kutoka Jangwa la Sini, ikisafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kama BWANA alivyoagiza. Wakapiga kambi huko Refidimu, lakini hapakuwa na maji ya watu kunywa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jumuiya yote ya Israeli ikaondoka kutoka Jangwa la Sini, ikisafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kama bwana alivyoagiza. Wakapiga kambi huko Refidimu, lakini hapakuwa na maji ya watu kunywa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mkutano wote wa wana wa Israeli ukasafiri, kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama BWANA alivyowaagiza, wakatua Refidimu; napo hapakuwa na maji, watu wanywe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kutoka jangwa la Sini, jumuiya yote ya Waisraeli ilisafiri hatua kwa hatua kama alivyoamuru Mwenyezi-Mungu, watu wakapiga kambi huko Refidimu. Lakini huko hakukuwa na maji ya kunywa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wao wote wa mkutano wa wana wa Isiraeli wakaondoka katika nyika ya sini kwenda safari zao kwa kuagizwa na Bwana, wakapiga makambi Refidimu, lakini maji ya kunywa watu hayakuwako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mkutano wote wa wana wa Israeli ukasafiri, kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama BWANA alivyowaagiza, wakatua Refidimu; napo hapakuwa na maji, watu wanywe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutoka jangwa la Sini, Waisraeli wote pamoja wakasafiri hatua kwa hatua kama vile Yawe alivyoamuru. Watu wakapiga kambi kule Refidimu. Lakini kule hakukukuwa maji ya kunywa.