Exodus 17:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini baada ya muda, mikono ya Mose ilichoka. Kwa hiyo Aroni na Huri walichukua jiwe wakaliweka karibu na Mose naye akaketi. Kisha wakaishika na kuiinua mikono yake, mmoja akauinua mkono wa kulia na mwingine mkono wa kushoto. Hivyo mikono ya Mose ikabaki imara ikiwa imeinuliwa juu hadi jua lilipotua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mikono ya Musa ilipochoka, wakachukua jiwe na kumpa alikalie. Haruni na Huri wakaishikilia juu mikono ya Musa, mmoja upande huu na mwingine upande huu. Wakaitegemeza mikono yake ikabaki thabiti hadi jua lilipozama.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini baada ya muda, mikono ya Mose ilichoka. Kwa hiyo Aroni na Huri walichukua jiwe wakaliweka karibu na Mose naye akaketi. Kisha wakaishika na kuiinua mikono yake, mmoja akauinua mkono wa kulia na mwingine mkono wa kushoto. Hivyo mikono ya Mose ikabaki imara ikiwa imeinuliwa juu hadi jua lilipotua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mikono ya Mose ilipochoka, wakachukua jiwe na kumpa alikalie. Aroni na Huri wakaishikilia juu mikono ya Mose, mmoja upande huu na mwingine upande huu. Wakaitegemeza mikono yake ikabaki imeinuliwa mpaka jua lilipozama.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mikono ya Musa ilipochoka, wakachukua jiwe na kumpa alikalie. Haruni na Huri wakaishikilia juu mikono ya Musa, mmoja upande huu na mwingine upande huu. Wakaitegemeza mikono yake ikabaki thabiti mpaka jua lilipozama.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mikono ya Musa ililegea; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitengemaza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini baada ya muda, mikono ya Mose ilichoka. Kwa hiyo Aroni na Huri walichukua jiwe wakaliweka karibu na Mose naye akaketi. Kisha wakaishika na kuiinua mikono yake, mmoja akauinua mkono wa kulia na mwingine mkono wa kushoto. Hivyo mikono ya Mose ikabaki imara ikiwa imeinuliwa juu hadi jua lilipotua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mikono ya Mose ilipolegea kwa kuwa mizito, wakachukua jiwe, wakaliweka chini yake, apate kulikalia. Kisha Haroni na Huri wakaishikiza mikono yake, mmoja huku, mmoja huko; ndivyo, mikono yake ilivyopata nguvu, mpaka jua lilipokuchwa,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kisha muda, mikono ya Musa ikachoka. Kwa hiyo Haruni na Huri wakatwaa jiwe wakaliweka karibu na Musa naye akaikaa. Kisha wakaishika na kuiinua mikono yake. Mumoja akauinua mukono wa kuume na mwingine mukono wa kushoto. Hivyo mikono ya Musa ikabaki imara ikiwa imeinuliwa juu mpaka jua lilipotua.