Exodus 17:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo watu wakamnungunikia Mose wakisema, “Tupe maji ya kunywa.” Mose akawauliza, “Mbona mnaninungunikia? Mbona mnamjaribu Mwenyezi-Mungu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo wakagombana na Musa wakisema, “Tupe maji ya kunywa.” Musa akajibu, “Mbona mnagombana nami? Kwa nini mnamjaribu Mwenyezi Mungu?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa hiyo hao watu wakateta na Musa, wakasema, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia, Kwani kuteta na mimi? Mbona mnamjaribu Bwana?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo watu wakamnung'unikia Mose wakisema, “Tupe maji ya kunywa.” Mose akawauliza, “Mbona mnaninung'unikia? Mbona mnamjaribu Mwenyezi-Mungu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo wakagombana na Mose wakisema, “Tupe maji ya kunywa.” Mose akajibu, “Mbona mnagombana nami? Kwa nini mnamjaribu BWANA?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo wakagombana na Musa wakisema, “Tupe maji ya kunywa.” Musa akajibu, “Mbona mnagombana nami? Kwa nini mnamjaribu bwana?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa hiyo hao watu wakamnung'unikia Musa, wakasema, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia, Kwa nini mnaninung'unikia? Mbona mnamjaribu BWANA?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo watu wakamnungunikia Mose wakisema, “Tupe maji ya kunywa.” Mose akawauliza, “Mbona mnaninungunikia? Mbona mnamjaribu Mwenyezi-Mungu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, watu walipomgombeza Mose na kusema: Tupeni maji, tunywe! Mose akawaambia: Mbona mnanigombeza? Mbona mnamjaribu Bwana?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa hiyo hao watu wakateta na Musa, wakasema, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia, Kwani kuteta na mimi? Mbona mnamjaribu BWANA?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo watu wakamunungunikia Musa wakisema: “Utupatie maji ya kunywa.” Musa akawauliza: “Mbona munaninungunikia? Mbona munamujaribu Yawe?”