Exodus 17:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mahali hapo Mose akapaita “Masa” na “Meriba”, kwa sababu Waisraeli walimnungunikia na kumjaribu Mwenyezi-Mungu wakisema, “Je, kweli Mwenyezi-Mungu yu pamoja nasi?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye akapaita mahali pale Masa na Meriba, kwa sababu Waisraeli waligombana na kumjaribu Mwenyezi Mungu wakisema, “Je, Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi au la?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akapaita mahali pale jina lake Masa, na Meriba; kwa sababu ya mateto ya wana wa Israeli, na kwa sababu walimjaribu Bwana, wakisema, Je! Bwana yu kati yetu au sivyo?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mahali hapo Mose akapaita “Masa” na “Meriba”, kwa sababu Waisraeli walimnung'unikia na kumjaribu Mwenyezi-Mungu wakisema, “Je, kweli Mwenyezi-Mungu yu pamoja nasi?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye akapaita mahali pale Masa na Meriba, kwa sababu Waisraeli waligombana na kumjaribu BWANA wakisema, “Je, BWANA yu pamoja nasi au la?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye akapaita mahali pale Masa, na Meriba kwa sababu Waisraeli waligombana na kumjaribu bwana wakisema, “Je, bwana yu pamoja nasi au la?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akapaita mahali pale jina lake Masa, na Meriba kwa sababu ya ugomvi wa wana wa Israeli, na kwa sababu walimjaribu BWANA, wakisema, Je! BWANA yu kati yetu au sivyo?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mahali hapo Mose akapaita “Masa” na “Meriba”, kwa sababu Waisraeli walimnungunikia na kumjaribu Mwenyezi-Mungu wakisema, “Je, kweli Mwenyezi-Mungu yu pamoja nasi?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akapaita Masa na Meriba (Majaribu na Magomvi), kwa kuwa wana wa isiraeli walimgombeza hapo, wakamjaribu naye Bwana wakisema: Je? Bwana yumo katikati yetu au hayumo?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akapaita mahali pale jina lake Masa, na Meriba; kwa sababu ya mateto ya wana wa Israeli, na kwa sababu walimjaribu BWANA, wakisema, Je! BWANA yu kati yetu au sivyo?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pahali pale Musa akapaita “Masa” na “Meriba”, ni kusema “Ujaribu” na “Magombano”, kwa sababu Waisraeli walimugombanisha na kumujaribu Yawe wakisema: “Kweli Yawe yuko pamoja nasi?”