Exodus 18:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yethro akasema, “Na atukuzwe Mwenyezi-Mungu ambaye amewaokoa mikononi mwa Wamisri na kutoka utumwa wa Farao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yethro akasema, “Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, aliyekuokoa wewe kutoka mikononi mwa Wamisri na Farao, na aliyewaokoa watu kutoka mikononi mwa Wamisri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Yethro akasema, Na ahimidiwe Bwana aliyewaokoa na mikono ya Wamisri, na mkono wa Farao; aliyewaokoa watu hao watoke mikononi mwa Wamisri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yethro akasema, “Na atukuzwe Mwenyezi-Mungu ambaye amewaokoa mikononi mwa Wamisri na kutoka utumwa wa Farao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akasema, “Sifa na ziwe kwa BWANA, aliyekuokoa wewe kutoka mikononi mwa Wamisri na Farao, na aliyewaokoa watu kutoka mikononi mwa Wamisri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yethro akasema, “Sifa na ziwe kwa bwana, aliyekuokoa wewe kutoka mikononi mwa Wamisri na Farao, na aliyewaokoa watu kutoka mikononi mwa Wamisri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Yethro akasema, Na ahimidiwe BWANA aliyewaokoa na mikono ya Wamisri, na mkono wa Farao; aliyewaokoa watu hao watoke mikononi mwa Wamisri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yethro akasema, “Na atukuzwe Mwenyezi-Mungu ambaye amewaokoa mikononi mwa Wamisri na kutoka utumwa wa Farao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yetoro akasema: Bwana na atukuzwe aliyewaponya mikononi mwa Wamisri namo mkononi mwa Farao, kwa kuwa amewaponya watu hawa na kuwatoa mikononi mwa Wamisri!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Yethro akasema, Na ahimidiwe BWANA aliyewaokoa na mikono ya Wamisri, na mkono wa Farao; aliyewaokoa watu hao watoke mikononi mwa Wamisri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yetro akasema: “Atukuzwe Yawe ambaye amewaokoa toka katika mikono ya Wamisri na kutoka katika mukono wa mufalme wa Misri.