Exodus 18:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, akawateua watu wenye uwezo kati ya Waisraeli, akawafanya kuwa viongozi wa makundi ya watu elfu, watu mia, watu hamsini na watu kumikumi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa akawachagua watu wenye uwezo kutoka Israeli yote, akawafanya wawe viongozi wa watu, maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa akawachagua watu wenye uwezo katika Israeli yote, akawaweka wawe vichwa juu ya watu, wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, akawateua watu wenye uwezo kati ya Waisraeli, akawafanya kuwa viongozi wa makundi ya watu elfu, watu mia, watu hamsini na watu kumikumi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawachagua watu wenye uwezo kutoka Israeli yote akawafanya kuwa viongozi wa watu, maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa akawachagua watu wenye uwezo kutoka Israeli yote, akawafanya kuwa viongozi wa watu, maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa akawachagua watu wenye uwezo katika Israeli yote, akawaweka wawe vichwa juu ya watu, wakuu wa maelfu, na wakuu wa mamia, na wakuu wa hamsini hamsini, na wakuu wa kumi kumi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, akawateua watu wenye uwezo kati ya Waisraeli, akawafanya kuwa viongozi wa makundi ya watu elfu, watu mia, watu hamsini na watu kumikumi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo Mose akachagua kwa Waisiraeli wote watu wenye nguvu, akawaweka kuwa vichwa vya watu hawa, maana wakuu wa maelfu na wakuu wa mamia na wakuu wa hamsini na wakuu wa makumi,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa akawachagua watu wenye uwezo katika Israeli yote, akawaweka wawe vichwa juu ya watu, wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, akachagua watu wenye uwezo kati ya Waisraeli, akawafanya kuwa viongozi wa makundi ya watu elfu, watu mia, watu makumi tano na watu kumikumi.