Exodus 19:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena wewe utawawekea watu mpaka kuzunguka mlima. Utawakanya wajihadhari sana wasipande juu mlimani wala kuugusa mpaka wake. Yeyote atakayeugusa mlima, atauawa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Weka mipaka kuzunguka mlima kwa ajili ya watu, uwaambie, ‘Mwe waangalifu, msije mkapanda mlimani au kuugusa. Yeyote atakayeugusa mlima atauawa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe utawawekea mipaka watu hawa pande zote, ukisema, Jihadharini, msipande mlima huu, wala msiuguse, hata mapambizo yake; kila mtu atakayeugusa mlima huu, bila shaka atauawa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena wewe utawawekea watu mpaka kuzunguka mlima. Utawakanya wajihadhari sana wasipande juu mlimani wala kuugusa mpaka wake. Yeyote atakayeugusa mlima, atauawa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Weka mipaka kuzunguka mlima kwa ajili ya watu, uwaambie, ‘Mwe waangalifu, msije mkapanda mlimani au kuugusa. Ye yote atakayeugusa mlima hakika atauawa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Weka mipaka kuzunguka mlima kwa ajili ya watu, uwaambie, ‘Mwe waangalifu, msije mkapanda mlimani au kuugusa. Yeyote atakayeugusa mlima hakika atauawa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe utawawekea mipaka watu hawa pande zote, ukisema, Jihadharini, msipande mlima huu, wala msiuguse, hata pambizo zake; kila mtu atakayeugusa mlima huu, bila shaka atauawa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena wewe utawawekea watu mpaka kuzunguka mlima. Utawakanya wajihadhari sana wasipande juu mlimani wala kuugusa mpaka wake. Yeyote atakayeugusa mlima, atauawa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena uwakatie hawa watu mpaka wa kuuzunguka mlima na kuwaambia: Jiangalieni, msiupande mlima huu, wala msiuguse hapo chini yake! Kwani kila atakayeugusa mlima huu atakufa;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe utawawekea mipaka watu hawa pande zote, ukisema, Jihadharini, msipande mlima huu, wala msiuguse, hata mapambizo yake; kila mtu atakayeugusa mlima huu, bila shaka atauawa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena wewe utawawekea watu mupaka kuzunguka mulima kuwaambia wajilinde sana wasipande juu kwenye mulima wala kugusa mupaka wake. Yeyote atakayegusa mulima, atauawa.