Exodus 19:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mlima wa Sinai ulikuwa umefunikwa na moshi kwa kuwa Mwenyezi-Mungu alishuka juu yake katika moto. Moshi wa moto huo ulipanda juu kama moshi wa tanuri kubwa na mlima wote ulitetemeka kwa nguvu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mlima Sinai ulikuwa umefunikwa na moshi, kwa sababu Mwenyezi Mungu alishuka juu yake katika moto. Moshi wa moto huo ulipanda juu kama moshi kutoka tanuru kubwa, na mlima wote ukatetemeka kwa kishindo,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mlima wa Sinai wote pia ukatoa moshi, kwa sababu Bwana alishuka katika moto; na ule moshi wake ukapanda juu kama moshi wa tanuu, mlima wote ukatetemeka sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mlima wa Sinai ulikuwa umefunikwa na moshi kwa kuwa Mwenyezi-Mungu alishuka juu yake katika moto. Moshi wa moto huo ulipanda juu kama moshi wa tanuri kubwa na mlima wote ulitetemeka kwa nguvu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mlima Sinai ulikuwa umefunikwa na moshi, kwa sababu BWANA alishuka juu yake katika moto. Moshi wa moto huo ulipanda juu kama moshi kutoka kwenye tanuru kubwa na mlima wote ukatetemeka kwa nguvu nyingi,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mlima Sinai ulikuwa umefunikwa na moshi, kwa sababu bwana alishuka juu yake katika moto. Moshi wa moto huo ulipanda juu kama moshi kutoka kwenye tanuru kubwa na mlima wote ukatetemeka kwa nguvu nyingi,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mlima wa Sinai wote pia ukatoa moshi, kwa sababu BWANA alishuka katika moto; na ule moshi wake ukapanda juu kama moshi wa tanuri, mlima wote ukatetemeka sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mlima wa Sinai ulikuwa umefunikwa na moshi kwa kuwa Mwenyezi-Mungu alishuka juu yake katika moto. Moshi wa moto huo ulipanda juu kama moshi wa tanuri kubwa na mlima wote ulitetemeka kwa nguvu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mlima wote wa Sinai ulitoka moshi, kwa kuwa Bwana aliutelemkia kwa moto, nao moshi wake ukapanda, kama moshi wa tanuru, nao mlima wote ukatetemeka sana,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mlima wa Sinai wote pia ukatoa moshi, kwa sababu BWANA alishuka katika moto; na ule moshi wake ukapanda juu kama moshi wa tanuu, mlima wote ukatetemeka sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mulima wa Sinai ulikuwa umefunikwa na moshi kwa sababu Yawe alishuka juu yake katika moto. Moshi wa moto ule ulipanda juu kama moshi wa furu kubwa na mulima wote ukatetemeka kwa nguvu.