Exodus 19:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wote wakaitikia kwa pamoja wakisema, “Mambo yote aliyoyasema Mwenyezi-Mungu, tutayafanya.” Mose akamjulisha Mwenyezi-Mungu jibu hilo la watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wote wakajibu kwa pamoja, “Tutafanya kila kitu Mwenyezi Mungu alichokisema.” Naye Musa akarudisha majibu yao kwa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu wote wakaitika pamoja wakisema, Hayo yote aliyoyasema Bwana tutayatenda. Naye Musa akamwambia Bwana maneno ya hao watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wote wakaitikia kwa pamoja wakisema, “Mambo yote aliyoyasema Mwenyezi-Mungu, tutayafanya.” Mose akamjulisha Mwenyezi-Mungu jibu hilo la watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wote wakajibu kwa pamoja, “Tutafanya kila kitu BWANA alichokisema.” Naye Mose akarudisha majibu yao kwa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wote wakajibu kwa pamoja, “Tutafanya kila kitu bwana alichokisema.” Naye Musa akarudisha majibu yao kwa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu wote wakaitika kwa pamoja wakisema, Hayo yote aliyoyasema BWANA tutayatenda. Naye Musa akamwambia BWANA maneno ya hao watu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wote wakaitikia kwa pamoja wakisema, “Mambo yote aliyoyasema Mwenyezi-Mungu, tutayafanya.” Mose akamjulisha Mwenyezi-Mungu jibu hilo la watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu wote wakaitikia pamoja kwamba: Yote, Bwana aliyoyasema, tutayafanya. Naye Mose akampelekea Bwana majibu haya ya watu;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu wote wakaitika pamoja wakisema, Hayo yote aliyoyasema BWANA tutayatenda. Naye Musa akamwambia BWANA maneno ya hao watu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wote wakaitikia kwa pamoja wakisema: “Mambo yote Yawe aliyosema, tutayafanya.” Musa akamujulisha Yawe jibu lile la watu.