Exodus 2:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye akamjibu, “Nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu na mwamuzi wetu? Je, unataka kuniua kama ulivyomuua yule Mmisri?” Hivyo, Mose aliogopa na kufikiri, “Bila shaka jambo hilo limejulikana!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule mtu akamjibu, “Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu? Je, unataka kuniua kama ulivyomuua yule Mmisri?” Ndipo Musa akaogopa na kuwaza, “Jambo lile nililofanya lazima limefahamika.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yule akasema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu wetu, na mwamuzi juu yetu? Je! Wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri? Musa akaogopa, akasema, Kumbe! Jambo lile limejulikana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye akamjibu, “Nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu na mwamuzi wetu? Je, unataka kuniua kama ulivyomuua yule Mmisri?” Hivyo, Mose aliogopa na kufikiri, “Bila shaka jambo hilo limejulikana!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule mtu akamjibu, “Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mtawala na mwamuzi juu yetu? Je, unataka kuniua kama ulivyomwua yule Mmisri?” Ndipo Mose akaogopa na kuwaza, “Jambo lile nililofanya lazima limefahamika.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule mtu akamjibu, “Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu? Je, unataka kuniua kama ulivyomuua yule Mmisri?” Ndipo Musa akaogopa na kuwaza, “Jambo lile nililofanya lazima limefahamika.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yule akasema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu wetu, na mwamuzi juu yetu? Je! Wataka kuniua kama ulivyomwua yule Mmisri? Musa akaogopa, akasema, Kumbe! Jambo lile limejulikana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye akamjibu, “Nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu na mwamuzi wetu? Je, unataka kuniua kama ulivyomuua yule Mmisri?” Hivyo, Mose aliogopa na kufikiri, “Bila shaka jambo hilo limejulikana!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akajibu: Yuko nani aliyekuweka kuwa mkuu wa mwamuzi kwetu? Je? Wewe unataka kuniua nami, kama ulivyomwua yule Mmisri? Ndipo, Mose aliposhikwa na woga, akasema: Kumbe lile jambo limejulikana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yule akasema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu wetu, na mwamuzi juu yetu? Je! Wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri? Musa akaogopa, akasema, Kumbe! Jambo lile limejulikana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye akamujibu: “Nani aliyekuweka wewe kuwa mukubwa na mwamuzi wetu? Unataka kuniua kama vile ulivyomwua yule Mumisri?” Kwa hiyo, Musa akaogopa na kufikiri: “Bila shaka jambo hilo limejulikana!”