Exodus 2:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Farao aliposikia juu ya tukio hilo akakusudia kumuua Mose. Lakini Mose alimkimbia Farao, akaenda kukaa katika nchi ya Midiani. Siku moja, Mose alikuwa ameketi kando ya kisima cha maji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Farao aliposikia jambo hili, alijaribu kumuua Musa, lakini Musa akamkimbia Farao na kwenda kuishi katika nchi ya Midiani, akaketi kando ya kisima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Farao alipopata habari, akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia mbele ya Farao, akakaa katika nchi ya Midiani; akaketi karibu na kisima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Farao aliposikia juu ya tukio hilo akakusudia kumuua Mose. Lakini Mose alimkimbia Farao, akaenda kukaa katika nchi ya Midiani. Siku moja, Mose alikuwa ameketi kando ya kisima cha maji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Farao aliposikia jambo hili, alijaribu kumwua Mose, lakini Mose akamkimbia Farao na kwenda kuishi katika nchi ya Midiani, akaketi kando ya kisima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Farao aliposikia jambo hili, alijaribu kumuua Musa, lakini Musa akamkimbia Farao na kwenda kuishi katika nchi ya Midiani, akaketi kando ya kisima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Farao alipopata habari, akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia kutoka kwa Farao, akakaa katika nchi ya Midiani; akaketi karibu na kisima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Farao aliposikia juu ya tukio hilo akakusudia kumuua Mose. Lakini Mose alimkimbia Farao, akaenda kukaa katika nchi ya Midiani. Siku moja, Mose alikuwa ameketi kando ya kisima cha maji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Farao alipolisikia neno hilo, akamtafuta Mose, amwue; lakini Mose akamkimbia Farao, asimwone, akaenda kukaa katika nchi ya Midiani, akakaa kwenye kisima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Farao alipopata habari, akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia mbele ya Farao, akakaa katika nchi ya Midiani; akaketi karibu na kisima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye mufalme wa Misri aliposikia juu ya tukio hilo akakusudia kumwua Musa. Lakini Musa akamukimbia mufalme, akaenda kukaa katika inchi ya Midiani. Siku moja, Musa alikuwa akikaa kando ya kisima cha maji.