Exodus 2:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kwa vile hakuweza kumficha zaidi ya muda huo, alitengeneza namna ya kikapu cha mafunjo, akakipaka namna ya lami, akamtia huyo mtoto ndani. Kisha akakiweka kikapu kando ya mto Nili kwenye majani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini alipoona hawezi kuendelea kumficha, akamtengenezea kisafina cha mafunjo, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha kwenye matete kando ya ukingo wa Mto Naili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akampatia kisafina cha manyasi akakipaka sifa na lami, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka katika majani kando ya mto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kwa vile hakuweza kumficha zaidi ya muda huo, alitengeneza namna ya kikapu cha mafunjo, akakipaka namna ya lami, akamtia huyo mtoto ndani. Kisha akakiweka kikapu kando ya mto Nili kwenye majani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini alipoona hawezi kumficha zaidi, akamtengenezea kisafina cha matete, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha katikati ya matete kando ya ukingo wa Mto Nile.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini alipoona hawezi kumficha zaidi, akamtengenezea kisafina cha mafunjo, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha katikati ya matete kando ya ukingo wa Mto Naili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akamtengenezea kikapu cha mafunjo akakitaliza kwa sifa na lami, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka kwenye nyasi kando ya mto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kwa vile hakuweza kumficha zaidi ya muda huo, alitengeneza namna ya kikapu cha mafunjo, akakipaka namna ya lami, akamtia huyo mtoto ndani. Kisha akakiweka kikapu kando ya mto Nili kwenye majani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Asipoweza kumficha tena, akamchukulia sanduku ya mafunjo, akayaziba kwa udongo wenye utomvu mweusi na kuyapata lami, akamweka mtoto humo ndani; kisha akaiweka hiyo sanduku katika manyasi kando ya mto mkubwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akampatia kisafina cha manyasi akakipaka sifa na lami, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka katika majani kando ya mto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kwa vile hakuweza kumuficha zaidi ya muda ule, akatengeneza namna ya kikapu cha mafunjo, akakipakaa namna ya kabulimbo, akamutia yule mutoto ndani. Kisha akaweka kikapu kando ya muto Nili katika majani.