Exodus 2:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, binti Farao akashuka mtoni kuoga, na watumishi wake wakawa wanatembeatembea kandokando ya mto. Binti Farao akakiona kile kikapu katika majani, akamtuma mjakazi wake akichukue.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo binti Farao akateremka kwenye Mto Naili kuoga, nao wahudumu wake wakawa wanatembea ukingoni mwa mto. Binti Farao akaona kisafina kwenye matete, akamtuma mmoja wa wajakazi wake kukichukua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi binti Farao akashuka, aoge mtoni, na vijakazi wake wakatembea kando ya mto; naye akakiona kile kisafina katika majani, akamtuma kijakazi wake kwenda kukileta.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, binti Farao akashuka mtoni kuoga, na watumishi wake wakawa wanatembeatembea kandokando ya mto. Binti Farao akakiona kile kikapu katika majani, akamtuma mjakazi wake akichukue.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo binti Farao akatelemka mtoni Nile kuoga, nao wahudumu wake wakawa wanatembea ukingoni mwa mto. Binti mfalme akaona kisafina katikati ya manyasi, akamtuma mmoja wa mtumwa wake wa kike kukichukua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo binti Farao akateremka mtoni Naili kuoga, nao wahudumu wake wakawa wanatembea ukingoni mwa mto. Binti mfalme akaona kisafina katikati ya manyasi, akamtuma mmoja wa watumwa wake wa kike kukichukua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi binti Farao akashuka, aoge mtoni, na vijakazi wake wakatembea kando ya mto; naye akakiona kile kikapu katika nyasi, akamtuma kijakazi wake kwenda kukileta.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, binti Farao akashuka mtoni kuoga, na watumishi wake wakawa wanatembeatembea kandokando ya mto. Binti Farao akakiona kile kikapu katika majani, akamtuma mjakazi wake akichukue.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mara akatelemka binti Farao, aoge mtoni, vijakazi wake wakitembea kando ya jito. Yeye alipoiona hiyo sanduku katikati ya manyasi akatuma kijakazi wake mmoja kuichukua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi binti Farao akashuka, aoge mtoni, na vijakazi wake wakatembea kando ya mto; naye akakiona kile kisafina katika majani, akamtuma kijakazi wake kwenda kukileta.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, binti ya mufalme wa Misri akashuka kwenye muto kuoga na wajakazi wake wakakuwa wanatembeatembea kandokando ya muto. Binti ya mufalme akaona kile kikapu katika majani, akamutuma mujakazi wake akitwae.