Exodus 2:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Papo hapo dada yake yule mtoto akajitokeza, akamwambia binti Farao, “Je, niende nikakutafutie yaya miongoni mwa wanawake wa Kiebrania akulelee mtoto huyu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo dada wa huyo mtoto akamuuliza binti Farao, “Je, niende nikakutafutie mmoja wa wanawake wa Waebrania akulelee huyu mtoto?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi umbu lake mtoto akamwambia binti Farao, Je! Niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako, akunyonyeshee mtoto huyu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Papo hapo dada yake yule mtoto akajitokeza, akamwambia binti Farao, “Je, niende nikakutafutie yaya miongoni mwa wanawake wa Kiebrania akulelee mtoto huyu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo dada wa huyo mtoto akamwuliza binti Farao, “Je, niende nikakutafutie mmoja wa wanawake wa Kiebrania akulelee huyu mtoto?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo dada wa huyo mtoto akamuuliza binti Farao, “Je, niende nikakutafutie mmoja wa wanawake wa Kiebrania akulelee huyu mtoto?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi dada yake mtoto akamwambia binti Farao, Je! Niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako, akunyonyeshee mtoto huyu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Papo hapo dada yake yule mtoto akajitokeza, akamwambia binti Farao, “Je, niende nikakutafutie yaya miongoni mwa wanawake wa Kiebrania akulelee mtoto huyu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, umbu lake mtoto alipomwuliza binti Farao: Niende kukuitia mnyonyeshaji wa Kiebureo, akunyonyeshee mtoto?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi umbu lake mtoto akamwambia binti Farao, Je! Niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako, akunyonyeshee mtoto huyu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Palepale dada ya yule mutoto akajitokeza, akamwambia binti ya mufalme: “Niende nikutafutie yaya kati ya wanawake Waebrania akulelee mutoto huyu?”